Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Maraccana ilikuwa burudani tupu na Brazil walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 2 mfungaji akiwa Fred na dakika 44, Neymar akafunga bao la pili kwa shuti kali.
Kipindi cha pili, dakika ya tatu, Fred tena akafunga bao la tatu ambalo lilionyesha kumaliza matumaini ya Hispania ambayo baadaye Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti.
Mshambuliaji Neymar amepewa nyota wa mchezo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment