CHUI AKIWA KATIKA MAWINDO.
DEVON, UINGEREZA.
MAHARUSI wawili nchini Uingereza, wamepatwa na mshtuko baada ya mnyama Chui kuibuka pasipo wao kujua chochote wakati wakipiga picha katika bustani ya wanyama ya Paignto mjini Devon Uingereza.
Chui huyo alitokea wakati maharusi Andrew na Karma Madgwick, walipokuwa wemekwenda katika bust
ani hiyo kupiga picha baada ya ndoa yao kufungwa.
Wakati wana ndoa hao wakipiga picha katika bustani hiyo, hawakufikiria jambo lingine lolote zaidi ya wao kuzama katika mahaba mazito.
Hivyo wakati wakiwa katika mahaba ghafla akatokea chui huyo ambaye alivutiwa na vazi la bibi harusi ambalo lilikuwa jeupe.
Akizungumzia sakata hilo, mpiga picha wao alisema wakati wakiwa katika mazungumzo ghafla bibi harusi alishtuka kuona gauni lake likichezewa na chui huyo.
Hata hivyo mpiga picha huyo aliweza kupiga picha ya haraka kati ya chui na maharusi hao. Maharusi hao walifurahia na kusema kuwa ni kumbukumbu nzuri ya harusi yao.
CHANZO JAMBOLEO.

0 comments:
Post a Comment