BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZEE WA KIMILA WA WAISHAMBULIA FAMILIA YA MZEE NELSON MANDELA.

Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela akifurahia jambo na wajukuu zake wakati alipokuwa na afya njema.

AFRIKA YA KUSINI. 
WAZEE wa kimila wa Kabila la Xhosa, wamesema kuwa mgogoro kati ya Mandla na wanafamilia wengine wa Mandela wa kufukua mabaki ya miili ya watoto wa Rais huyo wa zamani, umeishusha hadhi mila na tamaduni za Kiafrika.

Phathekile Holomisa, kiongozi mkuu wa chama cha kimila cha Afrika Kusini alikaririwa akiukosoa vikali uamuzi huo wa kuipeleka kesi hiyo mahakamani badala ya kuutatua kwa mkutano wa kimila au Ibhunga.

“Ingekuwa ni vyema kama wangeifukua miili hiyo kitamaduni kwa kuwaita wazee wa kimila wa Kabila la Mad
iba badala ya kutumia mahakama ambayo sheria zake ni za kigeni na si za kwetu,”alisema Holomisa.

Holomisa aliongeza kuwa jambo baya zaidi ambalo wanafamilia hao wamefanya ni kushindwa hata kuwaita wazee wa kimila kusali na kuzungumza na wazee wa jadi ambao ni wamiliki wa mabaki hayo. 

“Ili ufukue miili na kuizika upya unahitaji kuchinja na kutoa kafara,kutengeneza pombe kwa mizimu,kuiomba na kuieleza kwa nini unahamisha mabaki ya miili hiyo hadi ikubali,”alisema Holomisa.

Wakati mgogoro wa wanafamilia ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela kuhusu mahali pa kuzika miili ya watoto wa Rais huyo ukihitimishwa na mahakama, madaktari wanaomtibu Madiba wamethibitisha kuwa kiongozi huyo hapumui kwa msaada wa mashine.

Ofisi ya Rais, Afrika Kusini ilithibitisha hilo juzi na kusema kuwa Rais Jacob Zuma alimtembelea Mandela Alhamisi mchana na kusema kuwa hali yake ni mbaya lakini hapumui kwa msaada wa mashine kama baadhi ya wanafamilia wa Mandela walivyowahi kukaririwa wakisema.

“Tunathibitisha kauli hii kwa mara nyingine kuwa Rais Zuma alimtembelea Mandela hospitalini na aliweza kuona hali yake ilivyo kwa sasa,” alisema msemaji wa Rais Zuma, Mac Maharaj.

Msemaji huyo alisema Mandela anatibiwa na jopo la madaktari bingwa kutoka Jeshi la Afrika Kusini,madaktari binafsi,wa umma na madaktari bingwa kutoka Vyuo Vikuu nchini humo.

Wanafamilia ya Tata Mandela waumbuana
Mthatha.Ugomvi ndani ya familia ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela umegeuka kuwa mfululizo wa mivutano ndani ya ukoo, ambapo juzi Mandla alimtuhumu mwanafamilia mwenzake kwa uzinzi na ulafi wa mali za babu yake.

Akizungumza kwenye televisheni katika matangazo yaliyorushwa moja kwa moja na kutazamwa na mamilioni ya watu, Mandla aliuthibitisha umma kwamba mtoto wake wa kiume, Zanethemba ni mtoto wa kaka yake Mbuso, baada ya kufanya uzinzi na mkewe (Mandla), Anais Grimaud ambaye amemtaliki.

“Mbuso alimpa ujauzito mke wangu,”alidai Mandla alipozungumza kwenye televisheni akiwa kijijini kwake Mvezo. 
CHANZO MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: