DAVID MOYES ameanza kazi rasmi leo ya kufiundisha klabu ya Manchester United.
Kocha huyo wa zamani wa Everton leo
asubuhi ndio ameanza rasmi kazi ya kuwa boss wa benchi la ufundi
la Manchester United akirithi mikoba ya msoctland mwenzie Alex
Ferguson.
Moyes aliwasili katika kituo cha mazoezi
cha Carrington mnamo saa mbili asubuhi akiendesha gari la alilopewa na
wadhamini wa klabu hiyo Chevrolet.
Makocha hawa watatu wanakuja kurithi
nafasi zilizoachwa wazi na Mike Phelan, Rene Meulensteen na Eric
Steele, ambao wote waliondoka baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson
mwezi May mwaka huu.
Makocha hawa watatu wote wamefanya
kazi na Moyes wakiwa Everton - na baada ya kuthibitishwa kwao Moyes
alisema: "Nimefanya kazi na Steve, Chris na Jimmy kwa miaka mingi na
nina furaha kwamba wameamua kuungana nami kwenye klabu hii kubwa.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment