Gazeti la Sunday People lilichapisha 'mafaili ya siri ya FBI' yakionesha Mfalme huyo wa Pop aliwatunza na kuwasumbua watoto kuanzia mwaka 1989, licha ya kusisitiza kwake kwamba alikuwa akipitisha nao muda tu.
Mafaili hayo yanadai nyota huyo wa pop aliyefariki dunia alikuwa 'anayevutiwa kufanya mapenzi na watoto wadogo' ambaye alikuwa akitazama picha za ngono wakati akimshambulia mvulana mmoja, akimsumbua nyota mmoja wa utotoni maarufu, kutomasa sehemu za siri za mvulana mmoja ndani ya jumba lake la faragha la sinema na kumpapasa mtoto mwingine ambaye mama yake 'hakujisumbua' kwa hilo.
FBI hawakupokea simu zilizopigwa na waandishi wa habari hiyo jana.
Wanasheria wa familia ya Jackson mpaka sasa wanasisitiza nyota huyo ameishalipa familia ya Jordan Chandler pekee, mwenye umri wa miaka 13, ambaye alidaiwa kudhalilishwa mwaka 1993.
Hatahivyo mpelelezi aliyekodiwa na Anthony Pellicano - jicho la faragha Jackson anadaiwa kumkodisha kwa kazi ya kuyeyusha madai ya udhalilishaji - amedai Jackson alikuwa 'muwindaji watoto mzoefu' ambaye aligharimia watoto anaodaiwa kuwadhalilisha kwenye shamba lake lililoko Neverland.
Sunday People linasema lina ushahidi kusaidia madai hayo ya wapelelezi.
Wakati Anthony Pellicano alipochunguzwa mwaka 2002 kwa kuwasaidia nyota wa Hollywood, FBI ilikamata mafaili yake, yakiwamo mengi kumhusu Jackson.
Haya yalihusisha mafaili ya kesi CADCE MJ-02463 na CR 01046 ambayo Sunday People inadai inayo.
Mafaili hayo yalidaiwa hayakupitishwa kwa waendesha mashitaka kwenye kesi yenye utata ya udhalilishaji dhidi ya Jackson mwaka 2005.
Ubainishaji huo wa kushitusha umekuja baada ya binti wa Jacko, Paris, mwenye miaka 15, hivi karibuni kujaribu kujiua kwa kukata vifundo vyake vya mkono.
0 comments:
Post a Comment