1.Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya
jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi
na vifaa tiba.
2. Hivi
karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa
dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari.
Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.
b. Mamlaka
imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje
ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo
Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika.
Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo,
kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.
c. Pamoja
na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na
Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European
Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo la
damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol)
nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata
matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa
kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.
3. Kufuatia
taarifa hiyo, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii
kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi
ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Aidha, tunawakumbusha
watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya
dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya
nchini.
4. Mamlaka
inasha+uri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadhari
za madhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,
kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni
pamoja na kutumia dawa mbadala.
5. Vilevile
wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata
ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) – Makao Makuu
S. L. P 77150
Dar-es-Salaam
Tanzania
Simu: +255 22 2450751
+255 22 2450512
Barua pepe: info@tfda.or.tz
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment