Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa
Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa ziara
ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani
Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.
Obama
ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake
rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais.
NA MPEKUZI
Rais
Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na
kisha Obama atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya
kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali hapo
baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha
hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya
kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme
Barani Afrika.
Mpango
huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia,
Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake
wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.
Karibu Barack Obama kanga pamoja na vitenge waliova wananchi wa waTanzania
Katika
ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini na
hatimaye nchini Tanzania Obama amekuwa akisisitiza suala la demokrasia
ambapo ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na
viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.
Katika
ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za
kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza
kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma
kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini
Marekani
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment