MWEZI Mtukufu wa Ramadhani umeandama jana kuashiria kuanza kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni mojawapo
ya nguzo tano za dini ya kiislamu.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
alisema jana: "kuwa lulingana na kalenda ya dini ya Kiislamu na mwezi
umeandama hivyo (leo)
Jumatano waumini wa dini ye kiislamu wapo katika funga.”
Sheikh huyo aliwataka waumini wa dini hiyo
kushika msingi ya dini
na kutekeleza yote yaliyo mema ambayo yanahimizwa wakati wa mfungo.
Pia Sheikh Salum aliwataka wafanyabiashara kuacha
kuutumia Mwezi Mtukufu kupandisha bei za vyak
ula na badala yake waongeze huruma kwa kujitahidi kuvuna thawabu badala ya dhambi katika kipindi hiki.
ula na badala yake waongeze huruma kwa kujitahidi kuvuna thawabu badala ya dhambi katika kipindi hiki.
“Pamoja na kuwa tunaingia katika mfungo wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani, kila mmoja ajitafakari kwanza kuzidisha ibada,
kufanya matendo mema na zaidi ni kudumisha amani ya nchi yetu…lazima
kuilinda na kuitetea amani yetu kwani ni bora kuilinda kuliko
kuipoteza.”
0 comments:
Post a Comment