GUMZO LENYEWE
Picha
hizo za Lowassa ambazo zimeenea mtandaoni, zimepokea maoni mbalimbali
huku wengi wakiwa na maswali yaliyokosa majibu ya moja kwa moja.
Hata
hivyo, asili ya picha hizo zilizombadilisha mwonekano Lowassa ni
mtandao mmoja wa kijamii ambao umetupia picha na maelezo kwamba, mbunge
huyo ambaye kasi yake ya kisiasa nchini haishikiki, alikuwa akipongezwa
na Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al
Badawi kwa kumvika joho na kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa
ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislam
Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza.
ENEO
LA TUKIO
Ishu hiyo ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa
Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza hivyo kuondoa utata kwamba, alivaa
vazi hilo na kuzama nalo msikitini kitendo ambacho baadhi ya watu
walisema si sahihi kama mheshimiwa huyo hajabadili imani yake. Lowassa
ni wa imani ya KKKT.NA GLOBAL PUBLISHER
ACHANGISHA FEDHA, AVUKA MALENGO
Katika
harambee hiyo, Lowassa aliyekuwa jijini humo sanjari na wafanyabiashara
wengine wa karibu yake, alifan
ikisha wadau kuchangia shilingi milioni 590 hivyo kuvuka lengo la milioni 500. Kwa hiyo shilingi milioni tisini zilizidi.
ikisha wadau kuchangia shilingi milioni 590 hivyo kuvuka lengo la milioni 500. Kwa hiyo shilingi milioni tisini zilizidi.
Kufuatia
hali hiyo, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na baadhi ya viongozi wa
Kiislam ili kuwasikia wanaliongeleaje tuko la Lowassa kuvaa vazi hilo.
SKU zilizopita kabla ya Mfungo
wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, picha za Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM,
Edward Lowassa akiwa amevaa mavazi ya Kiislam ya joho na hagali zimezua gumzo
kubwa kwenye jamii wengi wakitaka kujua kama Waziri Mkuu Mstaafu huyo amebadili
imani au la !.
Akizngumza na gazeti
hili juzi, Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba alisema kitendo
anachofanya Lowassa cha kusaidia jamii ni cha kiungwana na kinakubalika kwa
kuwa analisaidia taifa.
“Kusaidia jamii kunakubalika na kila mtu na tunataka
watu kama Lowassa wawe wengi katika nchi yetu. Narudia tena kusaidia jamii si
vibaya hata kidogo tuige mfano huo,” alisisitiza Mufti Simba.
SHEHE WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa
akizungumzia tukio hilo alisema ni jema kwa kuwa alichochangia Lowassa
kitasaidia jamii ya Watanzania.
“Mheshimiwa Lowassa amechangia redio na kama
itatumika vizuri taifa zima la Tanzania litafaidika. Amefanya jambo zuri ambalo
watu wengine wanapaswa kuliiga. Ieleweke hakuchangia ibada kachangia huduma za
jamii,” alisema shehe huyo.
SHEHE WA MKOA WA MWANZA
Naye Shehe wa Mkoa wa Mwanza ambako tukio la Lowassa
lilifanyika, Salum Hassan Fareji kwa upande wake alimpongeza kiongozi huyo kwa
uamuzi wake wa kuchangia redio hiyo kwa kufanya harambee iliyozaa matunda.
“Alichokifanya (Lowassa) ni faraja kubwa kwetu sisi kama viongozi wa Kiislam,
tunamuomba aendelee kuhudumia jamii,” alisema.
KIONGOZI WA SUNNI
Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff
Hussein Al Badawi amesema kitendo alichokifanya Lowassa ni thawabu kubwa kwa
Mwenyezi Mungu na amewataka watu wengine kuiga uungwana huo.
JAMII INASEMAJE?
Baadhi ya Watanzania waliozungumza na Risasi
Mchanganyiko kwa nyakati tofauti walisema kwao kiongozi kuchangia jamii ni
vyema tu, mbaya kama katika kuchangia huko atakuwa anapiga kampeni ya nafasi au
cheo anachokifukuzia.
“Mimi sidhani kama kuna tatizo, kiongozi yeyote
anatakiwa kuisaidia jamii, awe tajiri au wa kipato cha kawaida, tatizo litaibuka
kama kiongozi huyo atatumia nafasi hiyo kufanya kampeni,” alisema Slim Abood,
mkazi wa Kijitonyama Dar.
KUHUSU LOWASSA
Siku za hivi karibuni, Mheshimiwa Lowassa amekuwa
akifanya harambee mbalimbali kuchangia jamii. Maeneo ambayo amekuwa akiyagusa zaidi
ni nyumba za ibada na makundi ya akina mama, lakini hivi karibuni alikutana na
Machinga wa Jiji la Mwanza ambao aliwaahidi kuwajaza ‘mafedha’ kwa ajili ya
kujiinulia vipato vyao.
NI KUUSAKA URAIS ?.
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya watu wakivitumia vyombo
vya habari wamekuwa ‘wakitabiri’ kwamba, Lowassa anafanya harambee hizo kwa
lengo la kuusaka urais wa Tanzania mwaka 2015.
Hata hivyo, Lowassa mwenyewe hajawahi kuweka wazi
msimamo wa kugombea urais mwaka huo.
LOWASSA AZUNGUMZA NA RISASI MCHANGANYIKO
Baada ya yote, Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya
kuzungumza na Mheshimiwa Lowassa kwa njia ya simu ya kiganjani na kumuuliza
nini madhumuni yake ya kufanya harambee ya kuchangia redio hiyo ambapo alikuwa
na haya ya kusema:
“Nimeamua kufanya harambee ile kwa sababu ni redio ya
dini. Unajua unapochangia redio ya dini, yoyote ile maana yake itaweza kutoa
vipindi bora vya kuelemisha jamii yote.
0 comments:
Post a Comment