BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAANDALIZI: ARSENAL YATOA KIPIGO CHA NGUVU VETNAM.

Challenge: Arsenal's Bacary Sagna tackles Vietnam's Nguyen Anh Duc Shughuli: Beki wa Arsenal, Bacary Sagna akiupitia mpira miguuni mwa Nguyen Anh Duc wa Vietnam.

ARSENAL imeendeleza wimbi la ushindi mnono katika mechi za kujiandaa na msimu, baada ya leo kuifumua mabao 7-1 Vietnam XI kwenye Uwanja wa My Dinh mjini Hanoi.
 
Ushindi huo umemoa majibu kadhaa kocha Arsene Wenger, kwanza kama atashindwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia kabla ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, Olivier Giroud atatosha kwenye kampeni ya ushindi baada ya kufunga mabao matatu peke yake.
 
Pili, anaweza kumtumia Bacary Sagna katika beki ya kati itakapotokea dharula kama atakwama kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams baada ya beki huyo kulia wa Arsenal kucheza namba nzuri.
 
Na tatu, inayoweza kuwa muhimu kuliko zote, Jack Wilshere na kama yuko fiti kabisa kuanza msimu, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza leo tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei.


Mbali na mabao matatu ya Giroud, mabao mengine ya Arsenal leo yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
 
Kikosi cha Arsenal leo kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71, Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46, Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46, Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46
Watching it fly in: Olivier Giroud scores one of his goals against Vietnam
Olivier Giroud akifunga moja ya mabao yake.
Speedster: Alex Oxlade-Chamberlain was also on target during the 7-1 win
Alex Oxlade-Chamberlain pia alifunga jana
Battle: Vietnam's Pham Thanh Luong vies for the ball with Arsenal's Bacary Sagna
RATIBA YA MECHI ZA ARSENAL KUJIANDAA NA MSIMU
Julai 14 na Indonesia XI walishinda 7-0.
Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1.
Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi.
Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi.
Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni.
Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni.
Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: