HATIMAYE winga mshambuliaji wa Real madrid Cristiano Ronaldo
ameondoa uvumi wa muda mrefu uliokuwa ukimuhusisha na uhamisho wa kurudi
Manchester United kwa kudai kuwa mustakabali wake uko katika klabu yake
ya sasa, Real Madrid.Supastaa huyo wa Kireno alikiri wazi mapenzi yake kwa klabu yake ya zamani wakati United ambayo ilimuuza Real Madrid kwa pauni milioni 80 mwaka 2009 ikijaribu kumrubuni arudi katika Premier League.
Lakini akizungumza jana na gazeti la AS la Hispania alipokwenda kwenye tamasha mjini Monaco, Ufaransa, Ronaldo alisema: “(Manchester United) ni klabu ambayo imekuwa katika moyo wangu kwa muda mrefu. Kila mmoja anajua shauku niliyonayo kwa klabu hii. Lakini mustakabali wangu uko Real Madrid.
“Pale Madrid, tunaweza kufanya yote kushinda La Liga na Champions League. Pia natumaini kufuzu Kombe la Dunia na Ureno.”
Mapema wiki hii, Ronaldo aliiambia Sky Sports: “Kweli ‘ninaimisi’ soka ya Kiingereza. Kwangu ilikuwa ni sehemu ya miaka bora wakati nilipokuwa pale, kila mmoja anajua hilo. Manchester United bado ni klabu ambayo iko karibu na moyo wangu.”
Real inajaribu kwa nguvu zote kuhakikisha staa huyo mwenye miaka 28 anasaini dili jipa, lakini United inatumaini ukaribu wake na kocha wake wa zamani, Sir Alex Ferguson, ambaye sasa ni mkurugenzi katika klabu, utasaidia kumrudisha ‘nyumbani’.

0 comments:
Post a Comment