Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini ya
Wizara hiyo wakifuatilia mawasilisho ya bajeti yao Bungeni mjini Dodoma
DAR ES SALAAM.
SERIKALI imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
DAR ES SALAAM.
SERIKALI imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa
Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi
cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyum
bani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
bani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima
kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa
sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za
nishati, madini na taasisi za fedha.
Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa
nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye
nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.
“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi
wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara
maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.
Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari,
posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini
kitaanzia Sh150,000.
Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa
hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati
kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni
Sh130,000.
Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa
kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa
na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi
zitatakiwa kulipa Sh100,000.
Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri
wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa
mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini,
uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja
la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne
Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment