BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

U.W.T CCM KATA YA SABASABA KUPATA SH7.9MILIONI KATIKA MIRADI MINNE YA UZALISHAJI MALI MORO.

 Mwenyekiti wa CCM kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro Mudhihil Shoo akifafanua jambo wakati akizungumza na akinamama katika hafla ya kuweka mikakati ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uanzishwaji wa miradi ya umoja wa wanawake Tanzania wa kata hiyo yenye lengo la kuwainua na kujikwamua kiuchumi mkoani Morogoro. kulia ni Diwani viti maalum, Nuru Majikata na Kushoto ni Mwenyekiti wa Umja wa wanawake wa CCM kata ya Sabasaba Mariam Msisi.
Mwenyekiti wa CCM kata hiyo, Mudhihil Shoo akimsikiliza Diwani wa viti maalum Nuru Majitaka wakati akizungumza jambo katika hafla hiyo.



Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMUIYA ya wanawake wa CCM Tanzania kata ya Sabasaba inatarajia kupata kiasi cha Sh 7.9milioni kwa mwaka mara baada ya kuanzisha kwa miradi mbalimbali yenye lengo la kuwainua akinamama na kujikwamua kiuchumi mkoani Morogoro.

Akizungumza na viongozi wa Umoja wa wanawake Tanzania kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro Mweny
ekiti wa CCM kata hiyo mjini hapa, Mudhihir Shoo alisema kuwa endapo umoja huo utajipanga vizuri kwa kusimamia miradi ya akinamama ya kujikwamua na kiuchumi itasaidia kupata faida kiasi cha Sh4.3milioni mara baada ya kupata kiasi cha Sh7.9 milioni kwa mwaka.

Shoo alisema kuwa kazi iliyopo mbele yao ni namna ya kusimamia miradi hiyo baada ya kuanzishwa kwake na wakifanikiwa kusimamia vema miradi hiyo italeta tija hasa kwa umoja huo kuondokana na umasikini ndani ya chama na wanaumoja kwani nina imani itasaidia upatikanaji wa ajira.

“Nimeona mchanganua wetu wa miaradi yenu lakini cha msingi ni kujipanga namna ya kusimamia miradi hiyo na nimeona kama mtaenda vizuri mnatarajia kupata Sh7,950,000milioni kwa mwaka na faida halisi ni kiasi cha Sh3,620,000milioni mara baada ya kuanzisha miradi yenu lakini itasaidia pia upatikanaji wa ajira” alisema Shoo.

Miradi hiyo ni pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji, utengenezaji wa batiki, sabuni na uanzishaji wa benki za ushirika vijijini (VIKOBA) Tanzania ambapo kuanzishwa kwa miradi hiyo inahitajika kiasi cha Sh4,324,000milioni kutokana na mali ghafi mbalimbali.

Naye Diwani wa viti maalumu kupitia tiketi ya CCM, Nuru Majitaka alisema kuwa Umoja huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni upatikanaji wa fedha za uanzishwaji wa miradi hiyo ambapo kiasi cha Sh4.3milioni ili kuweza kuanza kazi ya uzalishaji.

Majitaka alisema kuwa tayari wanachama wametoa michango kiasi cha Sh98,000 ambapo ghalama za kuanzisha miradi ni Sh4,226,000 na kuomba wadau mbalimbali wakiwemo marafiki wa CCM, wafanyabiashara ndani na nje ya kata hiyo kujitokeza kuwasaidia ili akinamama waondokane na tegemezi ndani ya chama na mtu moja moja.

Lengo kuu la mpango huo ni kumwezesha mwanamke kuondokana na maisha duni, tegemezi na umasikini ili kujitegemea na kuondokana na umasikini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: