BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIKU YA MWANAMKE WA AFRIKA 2013 YAADHIMISHWA DAR

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan (Katikati), akiungana na akina mama wa Kitanzania, wakati wa kusherehekea siku ya Mwanamke ya Wafrika jijini Dar es Salaam jana. Katika sherehe hizo zilizoandaliwa na WiLDAF-Tanzania, zilitumika kujadili mapendekezo ya awali ya katiba mpya ya Tanzania katika kulinda haki za mwanamke.
Msanii maarufu wa Tanzania, Mrisho Mpoto a.k.a MJOMBA, akitoa ujumbe kwenye moja ya maonyesho ya kikundi chake kupamba sherehe hizo kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam Jumatano Julai 31, 2013
Wasanii wa kikundi cha "MJOMBA" wakifanya vitu vyao kwenye sherehe hizo

Baadhi ya akina mama waliohudhuria sherehe hizo wakiwa na nakala ya rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano 2013, ambayo walijadili vipengele kadhaa vinavyohusu haki za mwanamke

Wasanii wa kikundi cha MJOMBA, wakitumbuiza kwa ngoma

Mwenyekiti wa WiLDAF-Tanzania, ambaye pia ni mheshimiwa mbunge wa viti maalum kupitia chama cha upinzani CHADEMA, Naomi Amy Mwakyoma Kaihula, (Wapili kushoto), akinena jambo huku akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa WiLDAF, Dr. Judith Odunga (Wapili kulia) na mwanaharakati wa haki za binadamu, Profesa Ruth Meena (Kulia), ambaye alichokoza baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2013 vinavyohusu haki za wanawake ambapo akina mama waliohudhuria sherehe hizo walijadili na wakwanza kushoto ni Mwanasheria kutoka kituo cha haki za binadamu (LHRC), Anna Henga.

Sehemu ya akina mama waliohudhuria sherehe hizo mmoja akiwa na mwanaye
Ili kuonyesha majukumu mengi yanayomkabili mwanamke, mama huyu akiwa amembeba mtoto wa miezi mitatu na nusu, Najim Fadhil. Mama huyu hakupenda kupitwa na sherehe hizo
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: