NI BAADA YA KUTOKEA UTATA KUHUSU KODI HIYO, SOMA HAPA.Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya mawasiliano.Waziri wa Fedha wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, William Mgimwa.
Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa
kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya
mawasiliano.
Mbali na
Moat, pia baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi, walipinga
kodi hiyo kwa walichokieleza kuwa itaongeza mzigo wa ugumu wa maisha
kwa mtumiaji, hususan wa kipato cha chini.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alipozungumza na gazeti hili
jana, alisema mara baada ya Rais kutoa agizo, wizara husika zilikutana
kufanyia kazi agizo hilo.
"Rais
akishaagiza kinachofuata ni utekelezaji na sisi kesho yake tulianza
vikao na ninachoweza kukwambia tuko pazuri na tukikamilisha majadiliano
yetu, tutatoa taarifa," alisema Makamba.
Alisema
lengo ni kuangalia kama Serikali inaweza kupata Sh bilioni 178 kutoka
vyanzo vingine, iwapo itaamua kufuta kodi inayotokana na tozo ya Sh
1,000 kutoka kwenye laini za simu.
Hivi
karibuni, Rais Kikwete aliagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na
mawasiliano na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana kutafuta
jinsi ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.
Alitoa
maelekezo hayo baada ya kukutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu
za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel.
Rais alisema lengo kuu la
mkutano huo, liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh bilioni 178
ambazo zitapotea katika bajeti, iwapo kodi hiyo itafutwa na Serikali
kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/14.
Aliwaambia
wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa hawezi kuifuta moja kwa moja kodi
hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo
litakalotokeza, huku tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nakuombeni
kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja
tutafute namna gani tutajaza pengo hili la Sh bilioni 178, endapo
tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa
pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema Rais Kikwete.
0 comments:
Post a Comment