Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Fredrick Kriel
akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu
yeyote awapo Mgodini.
Meneja
Mkuu wa Masuala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya
Mantra Tanzania, Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo
wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya
wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo na kuweza kujionea na
kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
Mkuu
wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Khadija Palangyo
akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika
kusaidia jamii inayouzunguka mradi huo.
Baadhi
ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini
wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye
ameambatana na wanahabari hao, na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya
Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani, Khadija Palangyo.
Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya ofisi za Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
Wanahabari hao wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Fredrick Kriel
akitoa maelezo ya namna mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini. Kulia ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapunda na kushoto ni
Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza kwa makini.
Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na
Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium, uliopo kwenye Kijiji Mkuju,
Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma, Fredrick Kriel akitoa mada ya masuala
ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari
waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa
ya Selou na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uranium.
0 comments:
Post a Comment