kuongeza: “Hivi sasa uchunguzi unaendelea, lakini hatuwezi kuwa
kila siku ni uchunguzi tu na wakati mwingine uchunguzi umekuwa hauna
matokeo.”
Alisema watumishi kama hao hawafai kwa kuwa wanat
umia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha wao binafsi.
umia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha wao binafsi.
Mkutano wa Smart Partnership Dialogue ulifanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Julai Mosi mwaka huu.
Alisema walifahamu kuhusu ufisadi huo baada ya
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kueleza kuwa kuna utata kwenye fedha
hizo na kwamba kampuni tatu hewa zililipwa fedha wakati hazijasajiliwa
kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).
“Kuna kampuni kama tatu, hizi nasikia
zimeshachukuliwa hatua kwa kuwa ni hewa lakini bado... lazima CAG afanye
ukaguzi kwa hizo Sh8 bilioni,” alisema Sitta.
Sitta ambaye amekuwa akijipambanua kuwa ni mmoja
wa kundi la viongozi wanaopinga ufisadi, alisema watumishi wa jinsi
hiyo, hawafai kwa kuwa wanatumia nafasi muhimu kwa nchi kujinufaisha
binafsi.
“Pamoja na yote, kampuni zina watu, lazima na wao
wachukuliwe hatua. Wahusika wote ninaamini wanafahamika sasa isifikie
hatua tunaambiwa uchunguzi usiofikia mwisho,” alisema Sitta.
Hata hivyo, Balozi Sefue hakupatikana jana
kuelezea tuhuma hizo ambazo hivi karibuni ziliripotiwa na gazeti moja la
kila wiki kwani simu yake iliita bila ya majibu na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi hakujibu na baadaye simu yake haikuwa tena hewani.
Aendelea kuponda Serikali Tatu
Sitta aliendelea na msimamo wake wa kupinga
mapendekezo ya Tanzania kuwa na Serikali Tatu akisema wanaopigania hilo
wana masilahi binafsi.
Sitta ambaye aliwahi pia kuwa Spika wa Bunge,
alishawahi kutoa msimamo wake kuhusu Serikali Tatu kama
zilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Rasimu ya
Katiba akisema hakuna nchi duniani yenye utawala wa marais watatu na
endapo Tanzania itakuwa hivyo, itaweka rekodi ya kuwa ya kwanza.
Sitta ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa miongoni
mwa wanasiasa wanaotaka kuwania urais mwaka 2015, alisema Katiba ina
masilahi ya watu aina mbalimbali lakini hatari anayoiona ni kwa wale
wenye masilahi binafsi ambao wanaweza kuathiri mchakato huo kwa kuwa
wanafikiria urais. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment