Dk Vincent Kafuuza wa Kituo
cha Friends Polyclinic & Ambulance Service alisema siyo tu kuhusu suruali
za kubana, lakini nguo zozote za kubana siyo nzuri kuwa mavazi ya kila siku.
Alieleza kuwa mwili unahitaji
kupumua, hali ambayo hufanyika kupitia kutoka jasho kwenye vinyweleo kwenye
ngozi na jasho linatakiwa kukauka lenyewe taratibu.
Dk Kafuuza alisema ikiwa mtu
amevaa jinzi ya kubana au nguo ya ndani ya kubana, jasho litagandana kwenye
vinyweleo vya ngozi na wakati mwingine inaweza kusabab
isha magonjwa ya ngozi kama vile ‘fangasi’, maumivu ya mwili na
vipele katika mapaja na sehemu zingine za siri.
“Wanaume ambao wanavaa
suruali za kubana wana hatari ya kupunguza kiwango cha mbegu za uzazi.
Na wakati mwingine zinaweza
kupungua kwa kiwango kikubwa na kumfanya mwanamume ashindwe kumpa ujauzito
mwanamke,” alisema Dk Kafuuza.
Dk Kafuuza alisema suruali za
kubana zina kawaida ya kusukuma ndani sehemu zinazotunza mbegu za uzazi za
mwanamume, hali inayosababisha matatizo kama vile uvimbe na ngozi kubabuka.
Nguo
za ndani za kubana zinazuia kukuwa kwa mbegu za uzazi.
Wakati joto la kawaida la
mwili ni sentigredi 37, mfuko wa mbegu za uzazi wa mwanamume unahitaji kiwango
cha joto kati ya sentigredi 35.5 na 36 ili kufanya kazi katika hali ya kawaida.
Dk Charles Kiggundu ambaye ni
Mshauri wa Hospitali ya Mulago na Chuo Kikuu cha Afya cha Makerere, alisema
joto la mbegu za uzazi za mwanamume linaweza kuongezeka ikiwa mfuko unaozishika
utafifia ndani ya mwili kwa muda mrefu, kwa mfano kama mwanamume amevaa nguo ya
ndani ya kubana.
Kwa mujibu wa Dk Lawrence
Kazibwe wa Hospitali ya Mulago, alisema mbegu za uzazi za mwanamume ziko kwenye
mfuko maalumu kwa sababu zinahitaji kuwa zimepoa zaidi ya maeneo mengine ya
mwili, ili ziwe kwenye mazingira tulivu.
Alisema lengo hilo linaweza
kuvurugika iwapo mwanamume atavaa suruali ya kubana ambayo itazifanya mbegu za
uzazi zikose mawasiliano ya kawaida na sehemu nyingine ya mwili, ambayo ni
kupata joto linalotakiwa.
“Baadhi ya wanaume wanafikiri
kusafirisha mbegu za uzazi pekee kwa mwanamke ndiko kunawezesha mwanamke kupata
ujauzito, lakini urutubishaji hauwezi kutokea katika sehemu za kikeni,
kwa kuwa mbegu za uzazi
lazima zipite kwenye mrija unaotakiwa kukutana na mayai mengine.
Hivyo basi mbegu za uzazi
zinahitaji kuwa na nguvu na nyingi ili ziweze kuyafikia mayai ya kikeni na
kuwezesha kupata ujauzito,” alifafanua Kiggundu.
Kiggundu alisema; “Hebu
fikiria katika hali ambayo mbegu za uzazi ni chache na dhaifu! Hii ina maana
hazitaweza kurutubisha mayai ya kike.
Hivyo unaweza kutoa mbegu za
uzazi wakati wa tendo la ndoa, lakini hakuna ubebaji mimba utakaofanyika.”
Mbegu za uzazi ambazo ni
dhaifu, kama vile zile ambazo hazina mkia, zenye mkia mkubwa, zenye mkia mdogo,
zilizopinda kichwani na zile zenye mikia miwili, haziwezi kupenye kwenye mrija
wa kwenda kwenye mayai ya uzazi ya kike.
Imeandikwa na Noor Shija kwa
msaada wa mtandao.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment