BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FUMANIZI

Fumanizi hilo lilibuliwa ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania akiwa na mumewe. 
 “Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,” kilisema chanzo hicho.
 
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.NA BONGO UMBEYA
Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
 
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
 
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
 
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: