TASWIRA ya ajali
ya basi iliyouwa watu 41 na kujeruhi 33 katika eneo la Ntulele lililo kwenye
mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya.
Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha zaidi ya
abiria 60 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nair
obi kuelekea mji wa Homabay uliopo magharibi
mwa Kenya lilikosa mwelekeo na kupinduka mara kadhaa usiku wa kuamkia Alhamisi.
Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye walipokuwa
wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine 33 waliopata majeraha mabaya
wanaendela kupata matibabu kwenye hospitali tofauti nchini Kenya.
Akituma
rambirambi zake kwa familia za marehemu, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka
madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha
maisha ya Wakenya hayapotei kwa ajali za barabarani. (Picha na Nation)
0 comments:
Post a Comment