Makongoro
Oging' na Haruni Sanchawa wa GPL
VITA
kupinga madawa ya kulevya imeingia katika hatua nyingine, safari hii Kamanda wa
Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa
amejikuta katika wakati wa hatari baada ya kutumiwa meseji za vitisho kwa
maisha yake.Habari za uhakika zinadai kuwa, tan
gu vita hiyo ipambe moto, baadhi ya
watu wanaodaiwa ni vigogo wa biashara hiyo haramu wamekuwa wakimtumia ujumbe
mfupi wa maneno (SMS) wakisema ajiangalie wanaweza kumtoa uhai.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, watu hao wengine wanasema watatumia
risasi kumtoa uhai huku wengine wakidai watamchoma moto bila kufafanua ni moto
upi.
Taarifa nyingine za ndani zaidi zinadai kwamba, maisha ya Kamanda Nzowa
kwa sasa ni kama digidigi kwa vile anaishi kwa kujificha ili kukwepa kuonekana
kwenye hadhara lengo ni kukwepa kufanyiwa kitu mbaya.
Kuhusu wabunge kudaiwa kutajwa kwa wingi kwenye makundi ya wauza unga,
habari zinasema ndani ya moyo wa Nzowa ndiko kwenye majina hayo.
“Nataka kusema jambo moja, wabunge kweli wanatajwatajwa sana kujihusisha
na madawa ya kulevya, lakini nataka kukwambia kuwa Nzowa ana siri nzito,”
kilisema chanzo hicho.
Kilisema kuwa, ni yeye ndiye mwenye hayo majina na atakayeyapeleka kwa
wakubwa wake serikalini, hivyo iko sababu ya serikali kuhakikisha maisha ya
mzee huyo yanalindwa kama ya viongozi wengine wa kitaifa.
Agosti 28, mwaka huu, Ijumaa lilimtafuta Kamanda Nzowa na kufanikiwa
kukutana naye uso kwa uso ofisini kwake, alipoulizwa kuhusu kutishiwa maisha
alikiri.
“Ni kweli, nimekuwa nikitumiwa meseji za vitisho kila mmoja akisema lake.
Wengine wanasema wataniua kwa risasi, wengine kwa moto sijui.
“Ni mambo mengi ziwezi kuyasema kwani siogopi mtu, mimi naitumikia nchi
yangu. Wewe si unaona siku hizi, unadhani mtu anaweza kutembea na madawa ya
kulevya kifua mbele kama zamani?” alihoji Kamanda Nzowa.
Ijumaa: Lakini kamanda unapata ulinzi wa kutosha? Maana kwa hii shughuli
yako unatakiwa kulindwa sana.
Nzowa: Ulinzi ni wa kawaida, lakini sehemu kubwa ya maisha yangu ulinzi
namwachia Mungu kwa sababu anasema yeye asipoulinda mji waulindao wakesha bure.
Kamanda
Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuwaonesha mapaparazi wetu maandiko kwenye
Kitabu Kitakatifu cha Biblia Agano la Kale katika Zaburi ambapo kunazungumzia
mtu awe anamtumaini Mungu katika ulinzi.
0 comments:
Post a Comment