Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye.
BUKONA.
SASA ni dhahiri kwamba kuna mvutano baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera na taifa kuhusu kufukuzwa uanachama kwa madiwani wake wanane katika Manispaa ya Bukoba.
SASA ni dhahiri kwamba kuna mvutano baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera na taifa kuhusu kufukuzwa uanachama kwa madiwani wake wanane katika Manispaa ya Bukoba.
Mvutano huo unadhihirishwa na kauli iliyotolewa
jana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Costansia Buhiye ambaye ametetea
uamuzi wa kuwatim
ua madiwani hao, huku Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akisema wameitisha mafaili yenye nyaraka zinazoeleza jinsi uamuzi huo ulivyofikiwa.
ua madiwani hao, huku Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akisema wameitisha mafaili yenye nyaraka zinazoeleza jinsi uamuzi huo ulivyofikiwa.
Kinana akizungumza na gazeti hili jana kwa simu
kutoka Arusha alisema: “Tayari katibu wetu wa mkoa ametuletea mafaili
yenye nyaraka zinazohusu suala hilo na suala hilo litapelekwa kwenye
kamati ya maadili na baadaye kuamuliwa na Kamati Kuu.”
Kinana alisema msingi wa suala hilo kuamuliwa na
vikao vya juu vya CCM unazingatia azimio lililowahi kupitishwa na vikao
vya chama hicho likielekeza kwamba uamuzi wa kuwafukuza wanachama ambao
waliochaguliwa na wananchi unapaswa kupata baraka za vikao vya juu.
Kauli ya Kinana inaunga mkono ile iliyotolewa juzi
na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye alisema madiwani
waliotimuliwa waendelee na kazi hadi vikao vya juu vitakapofanya uamuzi
wa mwisho na kwamba halmashauri ya chama hicho mkoani Kagera ilifanya
makosa kufikia uamuzi wa kuwafukuza.
Kauli ya Nape ndiyo iliyomfanya Buhiye jana
kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema haamini kama kauli ya
kupinga uamuzi huo imetolewa na kiongozi huyo wa kitaifa ambaye
anaifahamu vyema Katiba ya CCM inayowapa mamlaka hayo.
Buhiye alisema uamuzi wa kuwatimua madiwani hao
ulichukuliwa kwa wakati na muda mwafaka na kwamba lazima vikao vya chini
pia viheshimiwe kwani hakuna kikao chenye uhalali wa kufuta uamuzi wa
kikao kingine kilichofanyika kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
“Uamuzi wa kuwawajibisha madiwani ni sahihi na uamuzi wa vikao vya chini
lazima uheshimiwe.
Hata Halmashauri Kuu (Nec) ikikutana itarejea katiba ya chama chetu na kanuni zilezile tulizopitia,’’ alisema Buhiye.
Hata Halmashauri Kuu (Nec) ikikutana itarejea katiba ya chama chetu na kanuni zilezile tulizopitia,’’ alisema Buhiye.
Buhiye alisema amelazimika kuitisha mkutano huo
ili kupunguza shinikizo la wanachama aliodai wanataka kuandamana kutetea
uamuzi uliofanywa na uongozi wa CCM Mkoa.
“Nimewaita ili kutoa ufafanuzi sahihi nipunguze
shinikizo la wanachama wanaotaka kuandamana hadi hapa ofisini, wana
imani na Halmashauri Kuu ya Mkoa tuendelee kutulia,’’ alisema Buhiye.
Chadema yawaponda waliotimuliwa
Chadema Wilaya ya Bukoba Mjini kimewaponda
madiwani wa CCM waliotimuliwa kikisema wanastahili kutokana na kugomea
vikao kwa mwaka mzima, ikiwamo bajeti ya maendeleo ya wananchi. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment