JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni
majambazi tisa wa kutumia silaha akiwemo askari polisi wa kituo cha polisi
Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu.
Suleimani Kova
alisema kuwa majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo ambapo
pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)
zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi.
Aidha kamanda Kova
ameeleza pia wamekamata magari yanayosadikika kutumika katika uhalifu tofauti pamoja
na yenye namba za usajili T865CEH aina ya Carina, na T967 AUG Carina. CHANZO: ITV
0 comments:
Post a Comment