MCHEZAJI WA YANGA ATHMANI CHUJI AKIPAMBANA NA POLISI WAKATI AKITAKA KUMPIGA REFA CHUMBANI KWAKE MARTHIN SAANYA WA MOROGORO.
ASKARI Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, leo jioni.Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi.
Mwamuzi huyo Martin Saanya kutoka Morogoro alitoa penati katika dakika ya 90+ kwa kile kilichoon
ekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza kipenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.
Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kav
umbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo.
Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
Beki wa Coastal, Juma Nyoso (wa pili kushoto) akiondosha hatari, huku wachezaji wa Yanga, Hussein Javu (kushoto) na hamis Thabit, wakiwania mpira huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa Coastal.
Mabeki wawili wa Coastal, wakimdhibiti David Luhende.
Didier Kavumbagu, akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva. Katika mchezo huo mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Simon Msuva na wa Coastal.
Askari Polisi wakilinda mlango wa Chumba alichoingia Mwamuzi wa mchezo huo baada ya kuona usalama wake matatani, ambapo Chuji alijaribu kupangua ngome hiyo ili kuufikia mlango huo bila mafanikio. SUPHIANI MAFOTO BLOG
0 comments:
Post a Comment