Agosti 19, 2013 saa 2:12, Sheikhe Ponda alifikishwa Mahakama ya Kisutu, Dar akitokea Gereza la Segerea ambapo alifutiwa mashitaka ya kuchochea vurugu nchini kati ya Juni 2 na Agosti 10, mwaka huu kwenye maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Morogoro.
Kama hiyo haitoshi, siku hiyohiyo alikimbizwa Morogoro kujibu
mashitaka ya uchochezi aliyoyafanya katika mkutano wa hadhara hivi
karibuni mjini humo, hali ambayo ilimfanya atoneshe kidonda chake cha
risasi aliyodai kupigwa.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu, kutokana na jeraha hilo la risasi alilonalo kiongozi huyo, hekaheka alizozipata siku hiyo zilisababisha atoneshe kidonda na kumfanya ashindwe kusimama wala kulala hadi familia kufikia hatua ya kuomba arudishwe Hospitali ya Muhimbili katika kitengo cha mifupa (Moi) kwa matibabu zaidi.
“Kiukweli hali ni mbaya, wamempeleka harakaharaka tena ghafla,
matokeo yake wamemtonesha kidonda. Tunaomba wamrudishe tena Moi
(Muhimbili),” alisema mmoja wa ndugu wa familia aliyeomba hifadhi ya
jina.
Akiwa Morogoro, alipandishwa kizimbani na kujibu shitaka la kwanza la uchochezi pamoja na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Zanzibar. Agosti 10, mwaka huu kwenye mhadhara uliofanyika uwanja wa Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro, Ponda alidaiwa kuchochea kwa kusema:
“Ndugu Waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za
misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa
serikali.”
Shitaka hilo liliunganishwa na mengine mawili anayodaiwa kuyafanya Shehe Ponda maeneo ya Dar na Zanzibar.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment