Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo mjini Dodoma.
Katibu
wa NEC Uchumi na Fedha Zakhia Megji akibadilishana mawazo na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mama Salma Kikwete katika ukumbi wa NEC,
kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu Dodoma leo, 26 Agosti
2013.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za misiba
iliyojiri, kabla ya kikao akijaanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe
wa Halmashauri Kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kwa ajili ya
kumuombea mjumbe mwenzao aliyefariki ndugu Meja Jenerali Haji Makame
Rashid.
CCM YAZIDI KUWA IMARA ZAIDI
KIKAO Cha
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimemalizika jioni ya leo huku kukiwa na
mabadiliko mbali mbali makubwa kwenye chama hicho.
Kikao
hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa Jakaya Mrisho
Kikwete kimemalizika kukiwa na mabadiliko na mapendekezo mbali mbali,
kikao hicho ambacho kimekaa kwa siku tatu mfululizo kikitumia siku mbili mzika kujadili Rasimu ya Katiba na maoni ya wana CCM .
Halmashauri
hiyo pia imeridhia uamuzi wa kufukuzwa uanachama Mansour Yussuf Himid
kwa tuhuma za Kushindwa kusimamia malengo na madhumuni ya chama na
kutekeleza masharti ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa
mwanachama na kukiuka maadili ya Kiongozi wa CCM, Kuikana Ilani ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010-2015 na kukisaliti chama.
Mansour alianza uanachama tarehe 7/4/1988 na ni mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,wilaya ya Damani,Mkoa wa Magharibi Unguja.
katika
hatua nyingine ya Kimaadili sula la madiwani wa Bukoba bado halijafikiwa
uamuzi ingawa Kamati Kuu itakaa tena kesho tarehe 27 Agosti 2013
kufanya maamuzi ya suala la Bukoba.
Kamati
Kuu pia imependekeza majina ya Makatibu wa Jumuiya,Ikiwemo Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, Umoja wa Vijana CCM Ndugu
Sixtus Mapunda, Wazazi Seif Shaaban Mohamed .
Makatibu wapya wa Mikoa walioteuliwa ni Romuli Rojas John, Kaskazini Pemba Kassim Mabrouk Mbarak na Geita Mary Maziku.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment