Maktaba katika taasisi mbalimbali za elimu nchini Canada zimesheheni vifaa vya kusomea vya kisasa hususani kompyuta kama inavyoonekana katika maktaba hii ya Chuo cha Seneca kilichopo jijini Toronto. Picha na Abeid Poyo.
ELIMU ya Canada hailengi tu kuwapa wanafunzi maarifa,
bali inalenga pia kuwafanya wawe wabunifu, hasa katika kutoa mawazo
mapya na kutatua changamoto zinazow
eza kuhatarisha mafanikio ya nchi hasa upande wa uchumi.
Canada ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwamo elimu.
eza kuhatarisha mafanikio ya nchi hasa upande wa uchumi.
Canada ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikiwamo elimu.
Mwandishi wa makala haya, aliyeitembelea nchi hiyo
hivi karibuni, amezungumza na Dorris Ngaiza aliyewahi kusoma katika
mojawapo ya vyuo vikuu vya Canada, anayelezea sababu za nchi hiyo kupiga
hatua kubwa kielimu.
Swali: Ulisoma chuo gani na katika fani ipi?
Jibu: Nilisoma Chuo Kikuu cha
Carleton kilichopo Ottawa na kuhitimu mwaka 2012. Kozi niliyosomea ni
Shahada ya Kwanza ya Heshima katika Sheria na Sayansi ya Siasa. Katika
shahada hiyo, eneo kuu la utaalamu nililobobea lilikuwa Uhusiano wa
Kimataifa.
Swali: Unautazamaje mfumo wa elimu wa nchi hiyo ukilinganisha na ule wa Tanzania ?.
Jibu: Tofauti ni kubwa sana.
Elimu ya Canada imeendelea kwa kiwango kikubwa, hasa katika matumizi ya
vifaa vya kisasa na vya hali ya juu katika kufundisha na kujifunza.
Nilichokiona hapa ni kuwa mfumo wa wenzetu katika
ufundishaji unaweka msisitizo mkubwa katika mazoezi ya kivitendo, hivyo
kuchangia wanafunzi kuwa wabunifu na wenye uwezo wa kutatua matatizo.
Ilivyo ni kuwa wanafunzi hapa wanajengwa kuwa
werevu wa fikra na watatuzi wa changamoto, badala ya kuwa watu
wanaokariri tu maarifa wanayofundishwa.
Kwa ufupi naweza kusema elimu ya Canada hailengi
tu kuwapa wanafunzi maarifa, bali inalenga pia kuwafanya wawe wabunifu,
hasa katika kutoa mawazo mapya na kutatua changamoto zinazoweza
kuhatarisha mafanikio ya nchi hasa upande wa uchumi.
Swali: Tanzania nayo unaitazamaje ?.
Jibu: Kwa Tanzania hayo
niliyosema ni kinyume, kwani wanafunzi wanafundishwa ili kukariri
maarifa tena kwa minajili tu ya kufaulu mitihani ya Taifa.
Hali hii ndiyo inayochangia kukua kwa mawazo
potofu kuwa wanafunzi wenye akili, au wenye nafasi ya kufanikiwa
maishani ni wale tu wenye uwezo wa kufanya vizuri zaidi kwenye
mitihani. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment