BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIKI NDICHO KINACHOISUMBUA NCHI YA RWANDA KUHUSU KUICHOKONOA TANZANIA !!.

Historia ya Rwanda ni ndefu iliyojaa misukosuko ya kisiasa, kupinduana, vita na mauaji ya wenyewe kwa wenye yaliyosababishwa na ubaguzi wa kikabila.
Rwanda imekuwa ikipita katika vipindi vigumu na vya hatari. Vipindi hivi hufuatana na mauaji ya raia wa nchi hiyo, sio tu kutokana na sababu za ukabila bali pia uongozi mbaya wa kisiasa.
Mwaka 1959, mtawala wa Kit
utsi aliyekuwa akiitawala nchi hiyo na kulalamikiwa kuwa utawala wake ulikuwa ukiwaneemesha zaidi Watutsi walio wachache, uliangushwa na Wanyarwanda wa Kabila la Kihutu.
Mabadiliko haya yalifuatiwa na mauaji ya takriban Watutsi 150,000. Walioponea chupuchupu walikimbilia nchi mbalimbali jirani na Rwanda. 

Ni wakati huu wazazi wa Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame walikimbilia nchi jirani, Uganda yeye akiwa na umri wa miaka miwili.
Baada ya hapo, Wahutu wakaunda Chama cha PARMEHUTU, kikiongozwa na Gregoire Kayibanda, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Rwanda.
Mtu angedhani wakati huo kuwa kwa sababu uongozi wa nchi hiyo ulichukuliwa na kudhibitiwa na mtu kutoka kabila la Wahutu waliokuwa asilimia 88 ya Wanyarwanda wakati ule, (Watutsi wakiwa asilimia 11 na asilimia moja Watwa), kusingekuwa na chokochoko tena. Utawala ungekuwa wa amani, wapi?
Mapinduzi ya kijeshi
Kinyume na matarajio, Julai 5, 1973 Serikali hii nayo ilipinduliwa. Mapinduzi haya yalifanywa na jeshi la Wahutu wakiongozwa na Meja Jenerali Juvenal Habyarimana, ambaye naye alikuwa Mhutu.
Cha ajabu, licha ya tofauti hizo za kikabila, mapinduzi hayo yalifanywa na Wahutu walio wengi wakishirikiana na Watutsi wachache. Hii ilitokana na malalamiko kuwa Rais Kayibanda alikuwa akiendesha nchi kama familia yake, akipitisha uamuzi bila kushirikiana na viongozi wengine.
Baada ya mapinduzi hayo, kiongozi huyo mpya alibadilisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kusambaratisha chama kilichokuwa kikiongozwa na Kayibanda, PARMEHUTU, badala yake akaunda Chama cha National Revolutionary Movement for Development MRND.
Miaka takriban 17 baadaye kutokana na kile kilichoonekana kama utawala wa kikandamizaji, Watutsi waliokuwa nje ya nchi walishirikiana na Wahutu wa ndani kuanza harakati za kuiangusha Serikali ya Habyarimana.
Harakati hizi ndizo zilizomwingiza madarakani Rais wa sasa, Paul Kagame. Malalamiko kama yale yaliyosababisha mapinduzi dhidi ya mtangulizi wa Habyarimana yakajitokeza tena. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: