Omary Hamis akionyesha jeraha alilopata baada ya kudaiwa kupokea kipigo kutoka kwa askari wa jeshi la polisi mkoani Ruvuma.
Joseph Mwambije, SongeaJESHI la polisi mkoani Ruvuma limeingia lawamani baada ya askari wake kudaiwa kumshambulia, Omary Hamis mkazi wa Mfaranyaki Makaburini na kumvunja mara mbili mkono wa kulia na bega la kushoto na kumjeruhi maeneo mbalim
bali ya mwili wake baada ya kupigana na mkewe ambapo amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Askari wa jeshi hilo wanadaiwa kumshambulia
Omary Hamis mkazi wa Mfaranyaki Songea huku watoto wake wakishuhudia na
kumpiga kwa virungu na kumvunja mkono wa kulia na bega la kushoto na
kumsababishia majeraha mbambali kwenye mwili wake baada ya mwananchi
huyo kupigana na mkewe aliyewapigia simu polisi kutokana ugomvi
waliokuwa nao mke na mume.
Mtoto wa Abubakary Omary mwenye miaka 11 alishudia tukio hilo wakati baba yake ikipata kipigo hicho.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma,
George Chiposi alipofuatwa na ITV ofisini kwake kwa siku mbili mfululizo
aweze kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikana na alipotafutwa kwa
simu yake ya mkononi na kuelezwa kuhusiana na tukio hilo hakusema
chohote na kukata simu.
Mtoto wa Bwana Omary Hamis akiongea na ITV.
0 comments:
Post a Comment