DER ES SALAAM.
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (Moi), jana aliondolewa na kupelekwa katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam. Kitendo hicho kimelaaniwa vikali na familia yake na wafuasi wake, ambao wamepanga kufanya maandamano makubwa leo.

Sheikh Ponda, ambaye alisomewa shtaka la
uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Masht
aka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu.
aka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu.
Alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa.
Jana, Polisi waliimarisha doria kwenye Hospitali
ya Taifa Muhimbili kuanzia saa 1:30 asubuhi. Magari matatu ya Kikosi cha
Kutuliza Ghasia(FFU) yaliyobeba askari wenye silaha yalionekana
yakiranda katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Sheikh Ponda alitolewa wodini saa 4:20 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa askari baadhi yao wakiwa wamebeba silaha.
Alionekana akiwa ameshikiliwa na polisi kutokana na kukosa nguvu ya kutembea.
Akiwa amevalia shati lenye rangi ya udongo, kikoi
cheupe na kandambili, Sheikh Ponda alipakiwa kwenye gari ndogo aina ya
Landcruiser nyeupe lililokuwa na vioo vya giza.
Baada ya kupakiwa, safari ya kuelekea Segerea
ilianza saa 4:45. Gari lililombeba lilitanguliwa na gari la FFU
lililokuwa na askari wenye silaha likifuatiwa na magari mengine mawili
ya FFU yaliyokuwa na polisi wenye sare na magari mengine mawili ambayo
yalikuwa na askari kanzu.
Wakili ashangaa, familia yaja juu
Akizungumza baada ya tukio hilo jana, Wakili wa
Sheikh Ponda, Juma Nassoro alisema hakuwa na taarifa za kuondolewa
hospitali kwa mteja wake na kueleza kushangazwa na kitendo hicho akisema
mteja wake alikuwa mgonjwa akiwa anahisi maumivu makali ya kidonda
tangu juzi.
“Nimepigiwa simu mchana huu na mmoja wa
wanafamilia, nimeshangaa sana kwa sababu nakumbuka jana (juzi Jumatano)
Sheikh alishindwa kufanyiwa mahojiano na polisi kutokana na kuhisi
maumivu na kizunguzungu,” alisema Nassoro. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment