
azwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.
Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.
Serikali ya Kongo ilizikanusha mara moja tuhuma hizo, ikisema zilikuwa zikiashiria azma ya Rwanda kujiingiza waziwazi katika vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Kikomo cha uvumilivu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, amesema katika kipindi cha mwezi mmoja, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limerusha mabomu yapatayo 34 ndani ya Rwanda. ''Tumejizuia tuwezavyo kuchukuwa hatua, lakini sasa hatuwezi kuendelea kuvumilia uchokozi huu.'' Amesema Bi Mushikiwabo.
Kongo yasema ni kisingizio
Akijibu tuhuma kutoka Rwanda kuwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndilo linalorusha mabomu yanayoanguka nchini Rwanda, Waziri Mende amesema tuhuma hizo zinalenga kuhalalisha kujiingiza tena katika mikoa ya Kivu.
''Inachoazimia Rwanda ni kusababisha vurugu isiyokwisha ili iweze kuendelea kupora mali katika mikoa ya kivu, kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa miaka 15 iliyopita,'' alisema Mende.

Aidha, afisa wa ngazi ya juu wa MONUSCO, Ray Vilgilio Torres amesema vikosi vyao vimepata uhakika kuwa bomu lililomuuwa mwanamke nchini Rwanda, lilirushwa na waasi wa M23, kutoka ngome yao ya msitari wa mbele ya Kibati.
0 comments:
Post a Comment