WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa
Bunge), William Lukuvi amelazimika kufafanua kauli aliyoitoa juzi ya
kuhusisha wabunge na dawa za kulevya, kwa kusema hakumaanisha kwamba
wabunge wote ni wafanyabiashara wa dawa hizo.
Lukuvi ambaye jana alisisitiza kuwa Serikali haiko tayari kutaja
majina ya wafanyabiashara wa dawa hizo, aliliambia Bunge kwamba
alimaanisha ipo orodha kubwa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, yakiwemo
magazeti, vyenye majina na kwamba Serikali haiko tayari, kwa kuwa
inahesh
imu utawala wa sheria na mgawanyo wa majukumu.
Ufafanuzi huo aliutoa baada ya Mbunge wa Simanjiro , Christopher ole
Sendeka (CCM) kumtaka kutaja majina ya watuhumiwa, wakiwemo wabunge,
kama wapo, vinginevyo afute kauli yake, aliyoitoa bungeni juzi.
Akiomba mwongozo baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni,
Sendeka alisema kauli iliyotolewa na Lukuvi juzi, kwamba akitaja majina
ya wafanyabiashara ya unga, hakuna mbunge atakayepona ni ya
kulidhalilisha Bunge kwa kuwa Watanzania kwa kauli hiyo, wanawachukulia
wabunge kama wafanyabiashara hiyo.
“Naomba Mheshimiwa Waziri ataje majina hayo ili kuondoa mkanganyiko
kwetu wabunge mbele ya Watanzania, vinginevyo kauli hiyo inaweza
kuchukuliwa kwamba kila mbunge ni mfanyabiashara hii la sivyo afute
kauli yake ya jana (juzi) aliyotoa hapa bungeni,” alisema Sendeka.
Lukuvi alisema, “Serikali inaheshimu mihimili mingine ikiwemo Polisi
na Mahakama, hivyo si kazi ya Serikali kutaja tu majina kutoka kwenye
orodha ya watuhumiwa. Na hilo ndilo nililosema hapa bungeni jana (juzi).
Sikuamanisha kwamba wabunge ni wafanyabiashara ya madawa ya kulevya
bali nilisema katika orodha hiyo ndefu kutoka vyanzo mbalimbali, hata
wabunge waliomo humu ndani ya Bunge hili hawawezi kupona kutajwa,”
alisisitiza.
Kauli hiyo ya juzi ilitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM), Catherine Magige aliyetaka kufahamu sababu za biashara ya dawa
hizo kukithiri nchini, huku vijana wengine wa Kitanzania wakiendelea
kukamatwa kwenye viwanja vya ndege ndani na nje ya nchi. HABARILEO.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / KUSHINDWA KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI KUWATAJA WABUNGE WANAOJISHUHULISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA, YAWAKERA WABUNGE BUNGENI MJINI DODOMA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment