Jeshi la Congo FADRC baada ya kusambaratisha vikosi vya M23 huko Kibati.
KUNDI la M23 la jamhuri ya kidemokrasi ya kongo linasema linasitisha
mapigano na jeshi la Congo na kuondoka kwenye eneo ambalo mapigano
yalikuwa makali katika siku za karibuni ili kuruhusu uchunguzi huru
ufanyike kuhusiana na mizinga iliyoshambulia Rwanda .
Rwanda jana imeituhumu majeshi ya serikali ya congo kwa kufyetua mizinga
na roketi ndani ya ard
hi yake , lakini umoja wa mataifa na serikali ya
Kigali wanakilaumu kundi la M23 kwa mashambulio hayo.
Kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa aliiambia VOA kwamba
wapiganaji wake wanaondoka kwenye maeneo yao katika kijiji cha
Kanyaruchinya , karibu na Goma kwenye mpaka wa Congo na Rwanda ili
kuruhusu uchunguzi ufanyike kuamua nani hasa alihusika.
Naye msemaji wa majeshi ya serikali FARDC Olivia Amuli akizungumza na
VOA amesema kwamba wanajeshi wa serikali wamerudisha nyuma wapiganaji
wa M23 jana na M23 wameondoka kwasababu ya kupata pigo kubwa aliongeza
kuwa baada ya mapambano ya siku 9 hatimaye wamedhibiti maeneo ya
Kibati na Kilimanyoka na kusema waasi hao wamekimbia huku wakiwa
wameacha magari yao yaliopigwa na mabomu.
Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Congo alishiriki kwenye mjadala na
idhaa ya Kiswahili ya VOA msemaji huyo wa serikali alieleza kwamba M23
wamepiga mabomu huko Goma na nchini Rwanda ili wapate usaidizi wa Rwanda
huko Congo na sasa wameondolewa huko Kibati akidai kuwa M23
wanadanganya wananchi . Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.
http://www.voaswahili.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / M23 MAJI YA SHINGI, SASA WATAKA MAZUNGUMZO NA SERIKALI KUFUATIA KUSHINDWA KWAO MJINI WA GOMA NCHI KONGO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment