Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina.
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
“Wazungu
wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe
hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima
kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni
Mtanzania anayeishi China kwa sasa.Na GPL.sasa.Na GPL.
Aliongeza:
“Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya
kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito.
Kwa vile wanajua
Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.
“Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa.
Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China
kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.
“Kila
anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo
halali, anafunguliwa mashtaka. Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan,
nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu
wakikamatwa.
“Kote
hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa
msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine,
akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa
ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na
kugundulika siyo madawa ya kulevya.”
Habari
zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo
lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa
zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana.
Imebainishwa
zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika
wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale
msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.
Risasi
Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini
ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi
kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.
KINACHOWAPONZA NI HIKI.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na
sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali
ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na
hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la
kisigino.
Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.
“Punda
ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo
sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari
sana. Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.
“Vilevile
ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana.
Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe
unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi
Guangzhou, China.
CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA
Ripoti ya
Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012,
iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa
mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.
Amnesty
International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia
jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za
kunyonga watu bila mafanikio.
Shirika
hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga
watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.
BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi
mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman
Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la
Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa
wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli
hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu
hapa.
Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo
nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii
biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye
alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
0 comments:
Post a Comment