MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), amechafua hali ya
hewa bungeni kwa kuitaka Serikali kuwachukuliwa hatua viongozi wa juu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbunge huyo alisema
mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu wake, Dk.
Wilbroad Slaa, wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa madai ya kusababisha
mauaji ya raia.
Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bara, alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi
ilipotoka kwenye uchag
uzi, viongozi hao wamekuwa wakihamasisha
maandamano na kusababisha umwagaji wa damu za Watanzania.
“Mheshimiwa
Naibu Spika, katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi yetu
ilipomaliza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe na Dk. Slaa wamekuwa
wakitoa kauli za wazi na hata kusababisha mauaji ya watu bila hatia.
“Kutokana
na hali hii, sijui Serikali inafanya nini katika kuwachukulia hatua,
kwani viongozi hawa wamekuwa wakitafuta umaarufu wa kisiasa kwa
kuchochea chuki na mauaji dhidi ya raia.
“Kwa hali hiyo, tangu
kipindi hicho hadi leo hii wanasubiri nini badala ya kwenda kuwaweka
jela, kwani huko ndiko wanatakiwa kuwa,” alisema.
Mwigulu,
alisema kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya viongozi wa siasa, ambao
wamekuwa wakitumia majukwaa na kuhubiri umwagaji damu ni hatari kwa
taifa.
Alisema viongozi hao wamekuwa wakitumia majukwaa hayo na
kusababisha vifo vya wananchi, huku akitaja vurugu zilizotokea katika
mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na Singida.
Akijibu swali hilo,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, alisema
Serikali inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na
kukusanya ushahidi na kwamba mahakama ndicho chombo chenye uamuzi wa
mwisho dhidi ya adhabu kwa raia au kiongozi yeyote wa kisiasa.
Kauli
hiyo ya Mwigulu ilionekana kuchafua hali ya hewa ndani ya Bunge, ambapo
Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (Chadema), alisimama na kuomba
mwongozo wa Spika, huku akimtaka Mwigulu kuthibitisha kauli yake,
vinginevyo aombe radhi.
Wenje alisema hoja ya Mwigulu imekosa
mashiko na ina lengo la kuwadhalilisha viongozi wa Chadema, huku
akisahau kuwa baada ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki, aliyekuwa
Mwenyetiki wa Chadema tawi la Usa River, Omari Mbwambo, aliuawa na watu
anaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Awali katika swali la msingi,
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), alitaka kujua Serikali
inachukua hatua gani kwa wanasiasa wanaokiuka maadili na kusababisha
uvunjifu wa amani.
“Wanataaluma kama vile madaktari, wahandisi,
wahasibu na hata wakandarasi pindi wanapokiuka maadili ya kazi zao
huchukuliwa hatua kwa kufutiwa leseni zao.
“Vile vile viongozi wa
kisiasa wanayo maadili yanayowaongoza, kwanini pale wanapokiuka maadili
ya kazi zao hawachukuliwi hatua kama ilivyo katika makundi hayo?
(taaluma),” alisema Kilango. CHANZO MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MBUNGE WA IRAMBA AENDELEA KUICHOKONOA CHADEMA, ATAKA MBOWE NA DK SLAA WACHUKULIWE HATUA KUTOKANA NA MAUAJI YA RAIA HAPA NCHINI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment