GAZETI
la Morning Post la China Kusini limeripoti kwamba watu wazima nchini
humo wanawalipa wanawake fedha ili wawanyonyeshe maziwa yao ya kifuani !.
Wanawake wanaojitolea kutoa maziwa yao hulipwa kiasi cha dola 2,700
za Marekani (kama sh. Milioni 4) kwa mwezi ambapo watu wazima hao
huweza kuyanyonya maziwa hayo moja kwa moja kutoka vifuani mwa kinamama hao kama watoto wadogo !.
Watu wengi wanaona jambo hilo ni la ajabu kwa mwanamme au mwanamke mzima kunyonya matiti ya mwanamke mwenzake. Hata hivyo, nyuma ya kituko hicho kuna habari kwamba watu wanaofanya hivyo ni wale wenye magonjwa sugu na ambao wanashindwa kupata chakula kizuri chenye rutuba ya asili, badala ya vyakula vingi nchini humo ambavyo vimechakachuliwa.
Hivyo katika mazingira ya uchakachuaji huo ambayo yameenea nchini humo, watu wanakimbilia kwenye maziwa ya kinamama ambayo wanaona ndicho chakula halisi na cha asilia na chenye viini vingi vyenye kuimarisha afya ya binadamu.
Pamoja na hivyo, maoni ya watu ni kwamba iwapo watu wengine wanawakodisha kina mama hao kwa ajili tu ya kufanya kitu hicho kama burudani, basi kitendo hicho si cha kiungwana, lakini kama kweli wanafanya hivyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao, hatua hiyo ni jambo jema.
0 comments:
Post a Comment