JESHI la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu
wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni
mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa
Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na
wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo
kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO,
ambapo upanga huo ulikabidhiwa kw
a IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
a IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu
ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta
ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna
taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5,
2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa
na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya
kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya
SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo
hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila
mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa
kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP
aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa
kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa
Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP
alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita
kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita
mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi
upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali
Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti
wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya
kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya
Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa
hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja
na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema,
Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment