BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA WAKWAMISHWA TANZANIA, AFRIKA YA KUSINI KUWAFICHUA VIGOGO WA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KATI YA NCHI HIZO.

RAIS TANZANIA, JAKAYA KIWETE.
RAIS WA AFRIKA YA KUSINI, JACOB ZUMA.


DAR ES SALAAM/JOHANNESBURG
KUNA ushahidi kwamba Watanzania sasa ni makuli wa kubeba dawa za kulevya katika biashara haramu ambayo inazitaja Tanzania na Afrika Kusini kuwa miongoni mwa nchi ambazo ni njia kuu za kusafirisha dawa hizo.
Nchi hizo ni kama zina `ubia usio rasmi wa biashara hiyo’ na usafiri wa barabara unatajwa kuwa njia kuu ya usafir
ishaji wa dawa hizo, tofauti na viwanja vya ndege ambako Serikali na vyombo vya dola vimeelekeza nguvu za udhibiti.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya miezi miwili sasa hapa nchini na Afrika Kusini, umethibitisha kuwa baadhi ya Watanzania waliokamatwa nchini Afrika Kusini wamewataja vigogo wa dawa hizo, lakini nchi hiyo imeshindwa kuweka hadharani majina hayo kutokana na kuogopa kutetereka kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Orodha iliyopo katika taasisi za Serikali na vyombo vya dola nchini Afrika Kusini inawataja baadhi ya mawaziri waandamizi, wabunge na wafanyabiashara wakubwa kuwa wahusika wa biashara ya dawa hizo.
Uchunguzi uliofanywa katika Jiji la Johanersburg umebaini kwamba idadi kubwa ya Watanzania wanajihusisha siyo tu na usafirishaji wa dawa hizo, bali wengine wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na uvutaji au utumiaji wake.
Katika mitaa mikubwa ambayo waweza kuwakuta Watanzania katika jiji hili ni pamoja na Rissiki, CBD, Brii Taxi na vitongoji vingine vilivyo nje ya jiji kama Jeppestown ambako maisha yao ni ya taabu kwani wengi ni wachuuzi wa bidhaa ndogondogo lakini maarufu kwa biashara ya mihadarati.
Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Durban, Afrika Kusini, Edom Mwaikambo anasema ni Watanzania wachache wanaoishi kwa kufanya kazi za halali nchini humo kwani ‘wengi wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya’.
Kauli yake inaungwa mkono na taarifa ya Msemaji wa Ubalozi wa Tanzania, uliopo Pretoria, Habib Awesi aliyesema Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini hivi karibuni iliwasilisha majina ya Watanzania waliokamatwa kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba miongoni mwao ni Montana Silvery Kahindi na Amani Omary Emedi.
Awesi aliongeza kuwa sambamba na hilo ni Watanzania watatu waliouawa eneo la Belgravia, Cape Town kwa kile kinachohisiwa usaliti katika biashara za dawa za kulevya.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Luteni Jenerali Solomon Makgale alipoulizwa iwapo ana takwimu za Watanzania wanaokamatwa kwa makosa ya dawa za kulevya alisema jeshi hilo halitunzi rekodi zake kutoka na utaifa wa watuhumiwa bali kutokana na kosa.
Hata hivyo, Makgale alisema jeshi hilo linafanya kazi kwa ukaribu na polisi wengine ikiwemo Tanzania, ili kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inadhibitiwa. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: