DUMA.
Hakuna anayekimbia kwa kasi zaidi yake: duma wanaweza kufikia kasi ya
hadi kilomita 120 kwa saa. Ni jambo linaloendana na mazowea yao ya
kuwinda. Wanyama hao huwinda mchana, ambapo wanamnyemelea mnyama
mwingine na kisha kukimbia kwa kasi na kumkamata kwa kushtukiza. Hata
hivyo hawawezi kukimbia kwa muda mrefu na hivyo wasipomkamata swala
baada ya mita kama mia moja wanakata tamaa.SWALA"Pronghorn"
Hakuna anayekimbia kwa muda mrefu kama yeye: Pronghorn wanafikisha
kasi kati ya kilomita 60 hadi 70 kwa saa na wanaweza kukimbia umbali wa
kilom
ita tano. Mwili wao umezoea kukimbia mwendo mrefu kwa sababu moyo
wao kwa mfano una ukubwa mara mbili ya ule wa kondoo. Faida yake ni
kwamba wanaweza kuwakimbia wanyama wengine wanaotaka kuwakamata.MBUNI
Hakuna ndege anayekimbia kwa kasi zaidi yake: Kwake si tatizo
kukimbia kwa kasi ya kilomita 70 kwa saa. Anaweza kukimbia kwa nusu saa
kwa kasi ya kilomita 50 kwa saa. Ana miguu mirefu na misuli inayofaa kwa
kukimbia. Mbuni ni ndege pekee mwenye vidole viwili tu miguuni. Lakini
licha ya kuwa na mabawa makubwa, mbuni hawezi kupaa kwa sababu ya uzito
wake. TAI.
Hakuna anayepaa juu zaidi yake: Mwaka 1973 ndege wa aina hiyo
aligongana na ndege ya kubeba abiria iliyokuwa ikiruka mita 11,200 juu
ya usawa wa bahari. Aina nyingine za ndege zinaweza kupaa kufikia mita
100 hadi 2,000 tu. Lakini wapo pia ndege wanaolazimika kusafiri umbali
mrefu hali ya hewa ikibadilika na hao wakati mwingine hupaa mita 9,000
angani. Kwa mfano wakivuka milima ya Himalaya.
PUMA.
Hakuna anayeruka juu zaidi: Licha ya kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 50,
puma wanaweza kuruka juu urefu wa mita tano na nusu na kurukia mti.
Urefu huo unaweka rekodi kwa wanyama wanaonyonya na waishio ardhini.
Pomboo ni samaki pekee anayeruka juu zaidi kwani yeye anafikia mita
saba.NDEGE mdogo "Hummingbird"
Hakuna aliye mdogo zaidi: Jamii nyingi za ndege wa hummingbird ni
wadogo sana na ndio wanaoshikilia rekodi ya kuwa ndege wadogo zaidi
duniani. Wana urefu wa sentimita sita tu na uzito wa gramu mbili. Wakiwa
wanapaa, mabawa yao yanapiga mara 40 hadi 50 kwa sekunde.NYANGUMI.
Hakuna anayezama chini zaidi: Nyangumi huyu ni mnyama pekee
anayenyonya mwenye kuweza kuzama chini na kufikia kina cha mita 3000 na
kubakia majini kwa saa nzima. Hili linastaajabisha sana kwani nyangumi
lazima wavute pumzi. Mbinu yao ni kupelea damu katika viungo muhimu tu
wakiwa majini, yaani katika moyo na kwenye ubongo.CHOROA.
Hakuna anayestahili joto zaidi yake: Joto la mwili la nyuzi joto 45
halimsumbui. Binaadamu angekuwa ameshakufa kwenye joto kama hilo. Siri
yao ni kuwa na mishipa mingi ya damu katika shingo inayopooza mwili.
Pamoja na hayo, choroa hawahitaji kunywa maji mengi, mara moja kwa wiki
kadhaa inatosha.POPO.
Hakuna anayesikia vizuri zaidi: Popo wana masikio yanayosikia vizuri
kuliko wanyama wengine wote. Wakiwa wanapaa usiku, hutoa milio
isiyosikika kwa sikio la binadamu. Masikio yao hugeukia mwangwi wa sauti
hiyo na kwa njia hiyo wanaweza kuwakamata wadudu hata panapokuwa na
giza totoro.CHAWA.
Bingwa wa kuruka juu. Chawa anaweza kuruka urefu ulio hadi mara 200
ya ukubwa wake mwenyewe. Ipo aina moja ya chawa inayofikisha hadi mara
400 ya ukubwa wake.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment