Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye umri wa miaka
14 Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika kijiji cha Harambee wilaya ya Kakamega amejifungua watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana
wawili kati yao wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine
akiwa na uzito wa Kilogram 1.3.
Nesi wa zamu katika Hospitali ya
Bugoma Bi, Mary Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea
vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini hapo.
Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba Mzazi wa watoto
hao watatu waliozaliwa bado ni mtoto mdogo kama alivyo Mama yao kwani
Baba yao ana Umri wa Miaka 16 ambae pia bado anasoma.
Serikali ya Kenya imeondoa garama kwa wajawazito wakiwa
wanajifungua na hivyo kuweza kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo
Garama zozote zile.
WITO WETU KWENU TUUNGANE KWA PAMOJA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI, KWA KUTOA
ELIMU SITAHIKI NJISI YA KUEPUKA NGONO ZEMBE NA KUTUMIA KINGA.
0 comments:
Post a Comment