Mshambuliaji wa timu
ya soka ya Dodoma U17, Issa Abdi akimtoka mlinzi wa Tanga Erick Erick
wakati wa mchezo wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kituo
cha Morogoro katika uwanja wa jamhuri ambapo katika mchezo huo Tan
ga
ilitandikwa bao 1-0.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya vijana ya Temeke kutoka jijini la Dar es Salaam imefanikiwa kukusanya pointi tatu kutoka kwa wenyeji Morogoro wa mashindano ya Copa Coca Cola chini ya vijana wenye umri wa miaka 15 kwa kuitandika bao 2-0 katika mchezo mkali wa ufunguzi wa mashindano hayo kituo cha Morogoro uliofanyika majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Kipindi cha kwanza kilimazika kwa kutoshana nguvu ya 0-0 kutokana na kila timu kucheza kwa uangalifu huku safu za ulinzi zikifanya kazi lubwa ya kuwachunga washambuliaji wasilete madhara katika lango lao.
Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili vijana wa Temeke walikianza kipindi hicho kwa kasi na kutawala sehemu kubwa ya kiungo huku wenyeji wakionekana kuelemewa katika idara hiyo hali iliyowafanya kuruhusu mashambulizi katika lango lao na katika dakika ya 58 walinzi wa Morogoro walimruhusu mshambuliaji, Hamis Kajole kuipatia Temeke bao la kuongoza baada ya krosi ya kiungo, Yohana Mkomola na kujaza mpira wavuni kwa kichwa.
Morogoro walijaribu kujibu mashambulizi katika lango la Temeke wakitaka kusawazisha bao lakini safu yake ya ushambuliaji ilikosa umakini na kushindwa kutumia vema nafasi walizozipata kufumania nyavu na kujikuta wakipachikwa bao la pili dakika ya 69 na mshambuliaji, Hamis Kiduka.
Kiduka alifungaa bao hilo baada ya kuwalamba chenga safu ya ulinzi na kipa wa Morogoro kisha kukwamisha mpira kimiani na kuandika bao la pili na ushindi na kufanya mchezo huo kumalizika kwa wenyeji kukubali kipigo cha bao 2-0.
Naye Katibu Mkuu Mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka akizungumzia juu ya ratiba ya mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo yataendelea tena leo kwa timu ya vijana ya Morogoro kuchuana na Dodoma majira ya saa 2 asubuhi wakati Tanga ikicheza na Temeke katika mchezo wa utaofanyika saa 10 jioni katika uwanja huo wa Jamhuri.
Semka alisema kuwa vijana wa Morogoro baada ya kupoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Temeke kwa bao 2-0 itatupa karata kwa kujiuza dhidi ya Dodoma wakati Tanga nayo ikiwa na jukumu kama hilo baada ya yenyewe nayo kupoteza mchezo kwa Dodoma kwa kulala kwa bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment