WANYAMA na viumbe hai wengine barani Afrika wengi wako katika hatari ya kutoweka kabisa kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa na vitendo vya ujangili vinavyofanywa kila kona ya bara hili.
Pamoja na wanyama hao kuingizwa kwenye orodha ya wanyama walioko kwenye hatari na wanaohitaji uangalizi wa makini bado hali ya hatari ni kubwa kwa maisha yao na huenda katika miaka michache ijayo hawataonekana tena duniani.
Nimekuletea orodha ya wanyama kumi waliokwenye hatari ya kupotea barani Afrika, orodha ikijumuisha pia ndege ambao nao wako kwenye mstari mwekundu wa kupukutika.
1. Western lowland gorilla (Sokwe).
Idadi ya wanyama hawa imepungua kwa kiasi kikubwa sana na hii inatokana na ugonjwa wa Ebola ambao umek
uwa tishio kwa maisha yao. Kupungua kwa idadi yao ambako kunatajwa kuwa ni asilimia 60 pia kumesababishwa na kupungua kwa kuzaliana japo bado kunamatumaini ya kuongezeka katika siku za usoni.
uwa tishio kwa maisha yao. Kupungua kwa idadi yao ambako kunatajwa kuwa ni asilimia 60 pia kumesababishwa na kupungua kwa kuzaliana japo bado kunamatumaini ya kuongezeka katika siku za usoni.
Hii itafanikiwa tu endapo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kuwaepusha na majangili, wanyama hawa pamoja na kuishi katika hifadhi na mapori yanayolindwa na mamlaka za serikali bado wako katika hatari ya kuwindwa na majangili.
2. African penguin.
Kutokana na uvuvi haramu na uvuvi uliopitiliza (over-fishing) katika bahari ambako viumbe hawa wanaishi unaofanywa na wafanyabiashara wenye viwanda umechangia kupungua kwao kutokana na kukosa chakula na uharibifu wa mazingira. Sababu nyingine ni ile inayotokana na usumbufu wa shughuli za wanadamu ambapo hukwamisha uzalishaji hasa kwa kuwabughudhi ndege hawa wakati wa kuatamia na kuangua mayai. mbaya zaidi ni ukusanyaji wa mayai yao kwajili ya kutengenezea mafuta.
3. Black rhino.
Katika karne ya 20 wanyama hawa walikuwa wengi ukilinganisha na kipindi cha sasa ambapo wakati ule walikadiriwa kuwa 850,000 duniani kote. hata hivyo baada ya mwaka 1960 idadi yao ilipungua na kufikia 100,000 tu na hii ni kutokana na kuwepo kwa shughuli za kibinadamu na mambo ya ujangili kwa ujumla wake.
4. Ruppell’s vulture.
Mikasa mingi inawakumba ndege hawa, hasa tukianza na mkasa wa hivi majuzi ambapo waliwekewa sumu kwenye mzoga wa tembo na kupukutika kwa wakati mmoja zaidi ya tai 600, na hii ilitokana na tabia yao ya kuranda randa katika eneo lenye mizogo ambayo hutoa taarifa kwa askari wanyama pori kuwa kuna mnyama amekufa, hali ambayo inachangia kufichua vitendo vya ujangili.
5. Addax.
Wanyama hawa ndo kabisa idadi yao imepungua sana, kwa sasa inakadiriwa kuwa chini ya 300 na hii ni kutokana na kuwindwa sana. wanyama hawa wamekuwa nadra sana na kwa mara ya mwisho wameonekana huko Niger.
6. Southern ground hornbill.
Kwa Tanzania hawa ni salama kidogo bali madhara makubwa yako katika nchi kama Afrika Kusini ambako idadi yake imepungua sana. Ndege hawa wameuliwa sana kutokana na tabia yao ya kuvunja madirisha katika maeneo ya makazi lakini sababu nyingine ni kutokana na kasi ya ndogo ya kuzaana.
7. African wild dog (Mbwa mwitu).
Mbwa mwitu nao wamezidi kupungua kadri siku zinavyokwenda ambapo idadi yao sasa inakadiriwa kuwa 6600 pekee. kupungua kwa idadi hiyo kunatokana hasa na shughuli za kibinadamu, uwindaji haramu na magonjwa ambayo ama yanaenezwa kutoka kwa mbwa wa majumbani moja kwa moja au kwa kuambukizwa. Tabia ya wanyama hawa ni kumiliki eneo kubwa kwajili ya kufanya shughuli zao za mawindo na hifadhi nyingi zimeshindwa kuwalinda wanyama hawa kutokana na binadamu kujenga na kufanya shughuli zao karibu au ndani ya hifadhi. kuna hatari ya kuwapoteza wanyama hawa wasionekane kabisa katika miaka ya usoni.
8. Grey crowned crane.
Katika kipindi cha miaka 45 iliyopita (zaidi ya vizazi vitatu vya ndege hawa) kumekuwepo na upungufu mkubwa unaotokana na uhamishaji haramu wa mayai yao. mbali na hilo pia uvamizi katika maeneo mengi ya hifadhi hasa yenye unyevunyevu ambapo wakulima na wafugaji wanafanya shughuli zao kumesababisha wakose sehemu ya kuzalia. Ndege hawa wako hatarini zaidi kutokana na kutegwa na kuuzwa wakiwa wazima biashara ambayo imeshamiri kwa nchi za Tanzania, Uganda na Rwanda ambapo huuzwa nje ya nchi hasa katika nchi za arabuni. Ndege hawa hupenda kuishi karibu na makazi ya watu hivyo wengi wao wameuawa kwa kuwekewa sumu kutokana na tabia yao ya kula mazao.
9. African lion.
King of the jungle, Simba nae yuko kwenye hatari kubwa ya kutoweka kabisa kutoka idadi iliyokadiriwa ya 450000 miaka ya 1940 hadi kufikia 20000 kwa takwimu za sasa. wanyama hawa huuawa kwa uwindaji haramu, mauaji mengine hutokea pale watu wanapojilinda wao na mifugo yao, magonjwa na kuzaliana kwao kwa polepole.
10. Secretary bird.
Idadi ya ndege hawa imepungua sana na hii ni kutokana na kubughudhiwa na shughuli za binadamu, biashara ya ndege na mayai yake inayofanyika katika maeneo mengi ya hifadhi.
Ulimwengu wa leo ni wa kupashana na kubadilishana habari hivyo mwenye hoja na mawazo tofauti karibu kutoa maoni yako.CHANZO http://tabianchi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment