Askari wa bunge la jamhuri wa Muungano
wa Tanzania wakimdhibiti Mhe mbunge wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi a.k.a Suga ndani ya bunge wakati akitolewa ndani ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma jana.
Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF).
DODOMA.
JANA, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuh
udia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.

Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya
Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari
wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi
huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye
aliyeshambuliwa na askari huyo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job
Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe.
Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku akiwa hana viatu.
Pamoja na tafrani hiyo, Ndugai alisema wakati
akihitimisha kikao cha Bunge kipindi cha asubuhi kuwa amewasamehe
wabunge wote waliohusika na kosa hilo la utovu wa nidhamu na kuwaruhusu
kurejea kipindi cha jioni kuendelea na Muswada wa Marekebisho ya Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba.
Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.
Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.
Msimamo huo ulitolewa na Mbowe ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chadema, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na
Mbunge wa CUF, Habib Mnyaa.
Mbowe alisema wameamua kususia majadiliano hayo kuonyesha msimamo wao wa kupinga kupitisha mambo yasiyo na masilahi kwa nchi.
“Hatuko tayari kushiriki katika uchakachuaji wa
Katiba... Matumizi ya nguvu ya polisi kamwe hayatatupatia Katiba nzuri,”
alisema. Alisema kambi rasmi ya upinzani inalaani vikali kitendo cha
Ndugai kuruhusu Bunge kunajisiwa kwa kuruhusu polisi kuingia ndani
kinyume na kanuni.
Mnyaa alisema kitendo cha wadau wa Zanzibar
kutoshirikishwa katika kutoa maoni yao katika muswada huo wa marekebisho
ni dharau kubwa.
Mbatia alisema Tanzania haiwezi kuingia Uchaguzi
Mkuu wa 2015 kwa kutumia Katiba ya sasa kwa sababu tayari kuna mgongano
wa kikatiba kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu alimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kuu, (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi kutoa ushahidi kama Rais aliteua wajumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba kulingana na mapendekezo ya taasisi zao. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment