Mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi Mkalapa iliyoko wilayani Masasi akichota
maji kwa ajili ya kunywa katika bomba lililopo karibu na shule yao, wanafunzi wa kike wapaswa kupewa ulinzi kutokana na hatari zinazoweka kujitokeza dhidi yao, Picha hii haiusiani na tukio hili.
MATUKIO ya uvunjifu wa maadili
kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi
wanne wa Shule ya Msin
gi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa
kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea
kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wa kike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.
Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye
alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka
shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na
kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na
kumjulisha.
"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa
akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa
ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake
watatu," alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile
walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria
ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya
Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa
na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna
Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani
suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari
kusema mara taarifa zitakapokamilika.
"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado
haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa
shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara
baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi,
Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho
ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko
kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa
kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment