Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
DAR ES SALAAM.
WAKATI wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Kat
iba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
WAKATI wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Kat
iba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza
sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu
ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa
itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.
Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya
NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi
wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa
Katiba Mpya.
Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu,
muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge
Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa
ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete
anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni ?”.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni ?”.
Jaji Warioba pamoja na kukiri upungufu huo, alisema kurekebisha au kutokurekebisha kasoro hizo si jukumu la tume hiyo.
“Tunawaomba watafakari, waone jinsi gani tume
ambayo imekwishavunjwa itakuja kutoa elimu wakati wa kura ya maoni,
sheria ina ‘contradiction’ (ina mkanganyiko),” alisema.
Muswada huo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya
wale wa upinzani kutoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani,
Freeman Mbowe kuamuriwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutoka nje kutokana
na kukaidi kwake amri ya kukaa chini alipokuwa akitaka kutoa hoja kabla
ya mjadala wake kuanza.
Muswada huo unapingwa kwa kuwa Rais amepewa
mamlaka ya kuteua wajumbe 166, ambao si wabunge wala wawakilishi na
Zanzibar kutokushirikishwa kikamilifu kwenye maandalizi ya muswada huo.
Hata hivyo, Warioba alisema pamoja na kasoro hizo
Tume hiyo inafanya kazi yake kwa kufuata sheria hiyo huku akisisitiza,
“Wanaotunga sheria ni wengine siyo sisi, tulipoteuliwa tulikuta sheria
na kuanza kazi kwa kuifuata. Imefanyiwa marekebisho sisi tunafuata.”
Alisema waliofanya mabadiliko ya sheria hiyo wana
haki ya kufanya hivyo na kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi
kuzuia kutokufanyika kwa mabadiliko hayo, kwani yapo baadhi yanaihusu.
Alisema baada ya kuipata sheria hiyo: “Tulijiuliza
maswali kwa sababu miswada huwa inapelekwa bungeni na Serikali ikiwemo
ya Katiba. Anayeipeleka kama ni waziri ndiye anayetoa ufafanuzi pale
inapohitajika.”
Alisema kulingana na sheria, tume yake ndiyo
inayotakiwa kutoa ufafanuzi katika Bunge la Katiba, kama ambavyo Waziri
hutoa maelezo anapowasilisha muswada bungeni. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment