NI KAMA SINEMA LAKINI NDIYO HALI HALISI WATU 40 KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUPIGWA RISASI KUFUATIA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB KUVAMIA JUMBA LA MADUKA NA KUFYATUA RISASI OVYO NAIROBI NCHINI KENYA.
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliy
euawa, Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa huku 175 wakijeruhiwa. Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari Mashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana. Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo
Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao. September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine. Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa Maafisa wamesema watu hao wamebananishwa na kwamba watu wameshikiliwa mateka kwenye maeneo mbalimbali. Al-Shabab imeliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa limefanya shambulio hilo kujibu opereshini za kijeshi za Kenya zinazoendelea nchini Somalia.
Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silaha
Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine. “Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili.
Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabab
Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabab
Polisi wakipambana na Al-Shabab
Raia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao Wanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-Shabab Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne
wamekamatwa
0 comments:
Post a Comment