Wabunge wa Republikan wakitoa shutuma zao.
WAMAREKANI wameanza kuingiwa na wasiwasi na kuuliza lini mvutano wa
kisiasa utakapomalizika bungeni. Hii yote inatokana na kwamba siku ya
jumanne siku ya pili ya tangu kusit
a kwa sehemu kubwa ya kazi za
serikali wabunge walikuwa wakikashifiana.
Warepublikan walipendekeza mipango midogo midogo ya kutoa ili
kugharmia kufungua baadhi ya maeneo maarufu yanayoendeshwa na serikali.
Seneta Ted Cruz amehimiza kutolewa fedha za dharura kwa ajili ya maeneo
ya hifadhi za taifa na idara ya wanajeshi wa marekani waliostahafu.
Kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la seneti Harry Reid amesema wazo
hilo haliingi akilini. Seneta mwenzake wa chama cha Democratic Richard
Durbin aliieleza hiyo kuwa ni tusi kabisa.
Hadi kufikia mwisho wa siku utoaji mipango ya kutoa fedha kidogo kidogo
haukufanikiwa. Lakini kitendo hicho kilipelekea wademokrat katika nafasi
wasiyopenda ya kupinga kufungua sehemu ndogo ya shughuli za serikali na
hivyo kusaidia juhudi za warepublikan kujionyesha kuwa wao ni watu
wanaotaka kupatikana ridhaa ya maana na wademokrat kuonekana kuwa
wabishi.
Juhudi hizo zilianza mapema katika siku hiyo wakati baraza lililoongozwa
na warepublikan lilipopiga kura kutaka kuanza mazungumzo na baraza la
senet juu ya kufungwa kwa shughuli za serikali. Mbunge Mrepublikan Tom
McClintock amesema hivyo ndivyo Baraza la Wawakilishi linavyotakiwa
kufanya kazi.
Mvutano huo wote unatokana na sheria ya huduma za afya ya Rais Barack
Obama, sehemu kubwa ambayo imeanza rasmi jumanne.Warepublikan wametaka
kuondoa fedha au kuchelewesha utekelezaji wa sheria na warepublikan
wengi wamekataa kupiga kura kuidhinisha bajeti ya matumizi bila ya
kuwepo na vipengele vya kuharibu sheria hiyo ijulikanayo Obama care.
Maseneta Wademokrat wanasema wako tayari kufanya mazumgumzo ya pande
mbili lakini si wakati serikali imefungwa. Kiongozi wa walio wengi Harry
Reid, alitowa wito kwa wabunge kupitisha muswaada wa bajeti usio na
masharti yeyote ya kisiasa.
Uchunguzi wa awali wa maoni unaonyesha wengi wa wananchi wa Marekani
wanawashutumu Warepublikan kuliko Wademokrat na Rais Obama kwa kufungwa
kwa serikali.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment