Mwendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.Walter Barasa.
MAHAKAMA ya uhalifu ya kimataifa imetoa kibali cha kukamatwa kwa
mwandishi habari wa zamani anayeshut
umiwa kwa kutoa hongo kwa mashahidi
katika kesi ya naibu rais William Ruto .
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda alitangaza jumane kwamba
Kenya ilipata kibali cha kumkamata haraka Walter Barasa na kumpeleka
katika mahakama ya ICC mjini Hague.
Katika taarifa iliyorekodiwa Bensouda alisema Barasa alishiriki katika
kuingilia mashahidi kwenye kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya.
Anasema ushahidi uliokusanywa hadi Sasa unaonesha kuna mtandao wa watu
ambao wanajaribu kuvuruga kesi ya Ruto kwa kuingilia mashahidi upande wa
mashtaka ambapo Barasa ni mmoja wao.
Amesema kutolewa kibali hicho cha kukamatwa itakuwa onyo kwa wengine.
Kama atakutwa na hatia barasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka
mitano jela.
Amri ya kukamatwa ilitolewa Jumatano wakati naibu rais Ruto anakwenda
ICC kushiriki kuanza tena kusikilizwa kesi yake. Yeye na rais Uhuru
Kenyatta wanashitakiwa katika kesi tofauti za uchochezi wa ghasia za
mauaji baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2007.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / ICC YATOA KIBALI CHA KUKAMATWA KWA WANDISHI WA HABARI, KISA ANADAI KUVURUGA KESI YA NAIBU RAIS WA KENYA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment