MANCHESTER United hali imekuwa mbaya. Lakini, kocha wa zamani wa
kikosi hicho, Sir Alex Ferguson bado hajaondoa turufu yake kwa David
Moyes kwamba ataiw
eka sawa timu hiyo, huku akisisitiza kwamba hafikirii kurejea kuinoa timu hiyo ya Old Trafford.
eka sawa timu hiyo, huku akisisitiza kwamba hafikirii kurejea kuinoa timu hiyo ya Old Trafford.
Wataalamu wa masuala ya soka walikuwa wakimpigia
upatu mkongwe huyo arejee kunusuru mambo Manchester United baada ya sasa
kupoteza mechi tatu kati ya sita za mwanzo kwenye Ligi Kuu England na
kushika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Katika mahojiano na televisheni moja ya nchini
Marekani, Mskochi Ferguson alisema suala la kurejea kwenye kiti cha
ukocha wa Manchester United hilo haliwezi kutokea.
“Sivutiwi na kuwa kocha tena au kujihusisha na matokeo ya Manchester United kwa sasa,” alisema Ferguson.
“Manchester United ipo kwenye mikono salama ya
David Moyes. Atakuwa salama tu, yeye ni kocha mahiri. Utapoteza pesa
zako tu kwa kupiga kampeni za kutaka nirudi kuwa kocha.
Ferguson aliongeza: “Nimefanya uamuzi. Muda huu
ndiyo sahihi. Haiwezekani kwangu mimi kurejea kwenye ukocha. Nimeanza
maisha mapya kwa sasa.
Nataka kwenda kutazama Kentucky Derby na US Masters, Melbourne Cup. Nataka kutembelea Tuscany na Ufaransa.”
Kwenye mahojiano hayo na Charlie Rose, Ferguson
alibainisha kwamba alifuatwa na bilionea mmiliki wa Chelsea, Roman
Abramovich kumwomba aende akainoa timu hiyo ya Stamford Bridge.
“Walituma wakala wao aje kuzungumza na mimi pindi
Abramovich alipoinunua Chelsea kwa mara ya kwanza,” alisema Ferguson na
kuongoza:
“Niliwajibu hakuna kitu kama hicho.” Ferguson pia
aliibua upya sakata la straika Wayne Rooney baada ya kusisitiza kwamba
fowadi huyo alimfuata na kuomba kuhama Manchester United siku moja baada
ya klabu hiyo kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Hata hivyo, alisema amefurahishwa na namna straika
huyo alivyobadili msimamo wake na kucheza kwa kiwango kikubwa katika
kikosi hicho cha Manchester United kwa sasa. MWANASPOTI.
0 comments:
Post a Comment