BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KENYA KUFUNGA KAMBI ZA WAKIMBIZI NI BAADA YA KUJITOKEZA MAMBO YA UGAIDI KATIKA JUMBA LA MADUKA YA KIFAHARI YA WESTGATE MALL.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMod6sAwFpqc5PndtkRzVyYQ1XQo65KvqxHaDEYhcyIYFBU1ZPUq2i65epO3ObObPN3adqYaVrC6tHlo8Frs-avQ_mK7mrO6IPOxq-yvgNM8YSh4jEuydPzbfanXomIAZ-iAapt8fjEIXI/s1600/Uhurusmall.jpgRAIS UHURU KENYETTA.

SIKU chache baada ya magaidi wa Al Shabaab kuvamia jengo la Westgate na kuua watu kadhaa, Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Uhusiano na Mataifa ya Kigeni imepend
ekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini hapa ikisema zinafuga wapiganaji wa Kiislamu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ndungu Githinji alisema wana taarifa kuwa kambi zilizopo kwenye mipaka ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji hao.   Alisema Kenya inahifadhi wakimbizi wa Kisomali zaidi ya nusu milioni katika Kambi za Dadaab zilizopo kwenye mpaka na Somalia.

Mwenyekiti huyo aliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuwa miaka 22 imetosha kwa usaidizi kwa Wasomali hao na wanastahili kurudi nyumbani baada ya amani kurejeshwa nchini mwao.

“Hawa wakimbizi wamekaa miaka ishirini na mbili Kenya. Ningependa kuiomba Umoja wa Mataifa (UN) ifunge kambi hizo. Iwarudishe Wasomali kwao, maana sasa nao pia wana Serikali yao. Ili tuweze kukaa kwa amani,” alisema Githinji.   

Githinji pia alitoa mwito kwa vyombo vya usalama kuzidisha usalama na doria katika maeneo yanayotishiwa kushambuliwa na Al Shabaab.

“Tunasikia Al Shabaab wanasema kwamba bado wanataka kutupiga. Naomba kuwa zile sehemu zote walizotishia kushambulia zipewe ulinzi wa kutosha kwa saa ishirini na nne,” alisema Mwenyekiti huyo.

Wanamgambo wa Al Shabaab wamekuwa wakijihusisha na Waislamu katika harakati zao huku wakidai kuwa wanapigania haki ya dini ya Kiislamu nchini Somalia na katika mataifa jirani kama Kenya.

Pia wamekuwa wakilenga Kenya kwa mashambulio kutokana na hatua ya nchi hiyo kuingia nchini Somalia mwaka wa 2011 kuwaondoa wanamgambo hao kwa madai kuwa wanatishia usalama wa nchi.

Kutokana na hilo, wabunge waliozuru eneo la shambulio la Westgate wamefurahishwa na hatua ya Waislamu nchini Kenya kujiepusha na kundi hilo la Al Shabaab.

Mwenyekiti Githinji asema,” ningependa kupongeza viongozi wa Waislamu ambao wametoa taarifa yao kuwa hawaungi mkono mashambulio haya,”.

Mwandishi wa BBC jijini Nairobi alisema mwito wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma zimekuwepo kwa muda. Wakenya wengi wanahisi kuwa kuwepo kwa wakimbizi hao kumeendelea kuiweka nchi hiyo katika hatari ya mashambulio.

Hatua hiyo ya Bunge imekuja siku chache baada ya jengo la Westgate kushambuliwa na Al Shabaab na kuua watu takriban 67 na kujeruhi wengine wengi na kuharibu mali mbalimbali. Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo, Septemba 21, mwaka huu.

Wakati hali ikiwa hivyo nchini Kenya, ulinzi mkali umeimarishwa katika baadhi ya maeneo nyeti ya biashara hususan katika Jengo la Quality Centre ambapo mteja anayeingia katika eneo hilo analazimika kukaguliwa.

Ulinzi huo umeimarishwa ikiwa ni siku chache baada ya jengo la Westgate nchini Kenya kutekwa na Al Shabaab na kuua watu kadhaa. Hata hivyo, wateja wengi wanalalamikia kupekuliwa mabegi yao.

“Mimi ni Msomali lakini kinachonisikitisha ni kuwa nilipofika hapa Quality Centre kila mtu ananishaa…macho yote yapo kwangu kisa tu ni Msomali. Naomba Watanzania waelimishwe kwani si kila Msomali ni Al Shabaab,” alisema Fatma Abdallah.

Kwa upande wake, Erasto Mushi alilalamikia upekuaji huo akisema,” mtu anaweza kuwa na fedha nyingi hivyo kuwa katika hatari ya kuporwa na kuhatarisha pia maisha yake,”.   

Katika eneo la Mlimani City baadhi ya wenye maduka walilalamikia kutokuwa na ulinzi huku wakibainisha kuwa hata waliopo hawana vitendea kazi vinavyoeleweka katika kukabiliana na wahalifu.

“Hata nje magari yetu yanakuwa yanavunjwa vioo na kuibiwa,” alisema mmoja wa wenye maduka hayo huku akiomba wawekewe ulinzi kwa usalama wao na mali zao. Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwasiti Mwajasho aliambia gazeti hili kuwa baada ya Westgate kushambuliwa mzunguko wa biashara ulidorora.

“Ninachoshukuru sasa ni kuwa hali imebadilika kidogo, lakini nikiona Msomali ameingia ninashtuka…nikiwaona ninalazimika kuweka kitu kama boksi mbele yangu ili kujilinda,” alisema na kuomba Jeshi la Polisi liimarishe ulinzi eneo hilo. JAMBOLEO.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: